simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ajali … Moto Walipuka Kiwanda cha Kuku China

leave a comment »

Mmoja wa majeruhi

Mmoja wa majeruhi

Moto wataketeza kiwancha cha kuku China … Ajali

Moto uliotokea katika kiwanda cha kuku nchini China umeua watu wapatao 119, maofisa wanaohusika wamedokeza.

Moto huo ulitokea katika kiwanda cha kuchinja kuku huko Dehui katika jimbo la Jilini mapema Jumatatu.

Masimulizi yanaeleza kuhusu milipuko kabla ya kuzuka kwa mto huo, jambo lililowafanya wafanyakazi kuchanganyikiwa na kujikuta wakikanyagana wakati kila mmoja akitaka kujiokoa. Baadhi ya milango ya kutokea ilikuwa imefungwa kwa makufuri.

Hadi sasa inasemekana kwamba moto huo tayari umedhibitiwa na kazi ya kutoa miili ilikuwa ikiendelea.

Baadhi ya wasemaji, wakiwamo maafisa wa idara ya zima moto ya jimbo hilo, walieleza wasiwasi wao kwamba huenda kulikuwa na uvujaji wa gesi ya amonia jambo lililosababisha moto huo au kuukoleza moto huo na kuufanya ulete madhara makubwa zaidi.

Taarifa nyingine zinasema kwamba huenda kulikuwa na hitilafu ya umeme.

Picha za video za eneo hilo zinaonyesha mabaki yaliyoungua moto ya kiwanda hicho cha kuku.

Hili huenda ni tukio baya zaidi la moto nchini China tangu mwaka 2000, wakati huo kulikuwa na tukio lililoua watu 309 katika jumba la starehe maalumu kwa ajili ya muziki huko Luoyang, jimbo la Henan. Mwanaharakati mmoja wa haki za wafanyakazi aliiambia BBC kwamba tukio hili la moto lilikuwa baya kabisa katika historia ya matukio ya moto viwandani katika historia ya karne za hivi karibuni.

Karibu wafanyakazi 100 walifaulu kujiokoa kutoka kiwanda hicho ya Baoyuan, Xinhua ilisema, na kuongeza kwamba “jengo hilo ambalo kwa ndani linakanganya” pamoja na njia nyambamba za kutokea zilifanya suala la kujiokoa liwe gumu zaidi.

Habari zilisema kwamba lango la mbele la kiwanda lilikuwa limefungwa wakati mot ulipoanza.

Askari wa zima moto bado wanaendelea na kazi ya kuokoa miili kutoka kwenye jengo hilo, jambo linalomaanisha kwamba huenda idadi ya waliopoteza maisha itaongezeka, walisema baadhi ya mashuhuda.

Watu dazeni kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali kwa matibabu, lakini kwamba wameumia kiasi gani, ni jambo ambalo bado halijawekwa wazi.

Picha kutoka eneo la tukio zilionyesha paa lililoungua vibaya huku vyuma vya kenchi vikiwa vimepindika kutokana na moto mkali.

Serikali ya jimbo ilisema kwamba ilipeleka vikosi vyenye jumla ya askari wa zima moto 500 na madaktari 270 na manesi katika eneo hilo ili kuokoa na kuondoa watu, kwani eneo la jirani lina wakazi wapatoa 3,000, Shirika la habari la Reuters liliripoti.

Source: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

June 3, 2013 at 6:20 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: