simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ukwepaji Kodi … Nchi Changa Zayakabili Makampuni ya Kimataifa

leave a comment »

Wafanyakazi katika mgodi. Je, kuna uwiano wa kimapato kati ya kinachozalishwa katika migodi na kinachoingia katika mikono ya serikali kupitia kodi? Nchi nyingine zinazoendelea zinachukua hatua zipi? Soma habari hii.

Wafanyakazi katika mgodi. Je, kuna uwiano wa kimapato kati ya kinachozalishwa katika migodi na kinachoingia katika mikono ya serikali kupitia kodi? Nchi nyingine zinazoendelea zinachukua hatua zipi? Soma habari hii.


Ukwepaji Kodi: Nchi Zinazoendelea Zayakabili Makampuni ya Kimataifa

By Michael Robinson BBC News

Nchi zinazoendelea zinachukua hatua kukabili ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni makubwa ya kimataifa.

Zambia na Mongolia zimelieleza Shirika la Habari la BBC kuwa zinataka kuzuia utaratibu wa kampuni za uchimbaji madini kuhamisha faida yote kutoka kwenye nchi hizo kabla ya kutozwa kodi.

Nchi hizi mbili ni wazalishaji wakubwa wa madini na zinasema kwamba zinapoteza mabilioni ya dola kila mwaka ambazo nchi hizo zinahitaji kupitia kodi.

Hata hivyo, Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) limeonya kwamba hatua hizo zinaweza kuwa za hatari.

Shirika hilo la mataifa yaliyoendelea lenye makao yake jijini Paris, Ufaransa, linasema hatua za aina hiyo zinazofanywa na nchi moja moja zinaweza kusababisha mkanganyiko, sheria zisizoshikamana vema na kukosekana kwa viwango vinavyoeleweka vizuri.

Spika wa Bunge la Mongolia, Bw Z. Enkhbold, aliiambia BBC kwamba Mongolia ina mpango wa kufuta mikataba yote ya kimataifa ya mambo ya kodi ambayo makampuni ya uchimbaji madini yalikusudia kutumia ili kuhamisha faida kutoka nchini humo pasipo kulipa kodi ya uendeshaji.

“Kodi lazima ilipwe pale mahali inapoendeshwa biashara yenyewe halisi,” Bw Enkhbold aliiambia BBC, “na si katika nchi za ng’ambo”.

Athari itakuwaje

Sheria mpya nchini Zambia, ambayo itaanza kutumika mwezi huu, inataka makampuni yote ya uchimbaji madini kurejesha nchini humo ripoti kamili ya mauzo yanayofanyika. Baada ya ripoti hiyo kupelekwa Zambia, mamlaka ya mapato ya nchi hiyo itakagua gawio na malipo mengine ili kuona kama kuna uwiano halisi kabla ya faida hiyo kuhamishiwa nje ya Zambia.

“Hapa unazungumzia kuhusu wanawake wajawazito ambao hawana kliniki wanakoweza kwenda kwa ajili ya huduma za uzazi au elimu ya afya ya mtoto,” anasema Bw Guy Scott, Makamu wa Rais wa Zambia.

Makamu huyo wa Rais aliiambia BBC kwamba serikali yake inapoteza karibu dola bilioni 2 za Marekani kutokana na ukwepaji kodi ya uendeshaji kampuni.

“Tunazungumzia kiasi kikubwa sana cha fedha hapa,” alisema. Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuliko kile ambacho Zambia hutumia kila mwaka katika bajeti ya afya na elimu kwa pamoja.

“Unatazama watu ambao hawatapata elimu zaidi ya ngazi ya shule za msingi.”

Sheria mpya ya Zambia imeandaliwa katika namna inayohakikisha kuwepo kwa uwazi wa kimapato katika makampuni ya uchimbaji madini.

“Kwanza, hata hatujui akaunti hizo ziko wapi,” Bw Scott alieleza. “Walau sheria hii itafanya kuwa ni kosa la jinai kufanya ukwepaji wowote ule wa kulipa kodi. Inawalazimisha watu kuwa wawazi. Kwa sasa, wanakuwa wazi pale tu wao wenyewe wanapotaka kujitolea kuwa wazi.”

Chanzo: BBC News

Tafakari

Je, hali ya mambo iko vipi nchini Tanzania? Sekta ya madini ni miongoni mwa zinazochangia kwa kiasi kikubwa sana pato la nchi, lakini, je, kuna uwiano wa mapato kati kile kinachouzwa nje na kinacholipwa serikalini? Sheria zetu zinahakikisha uwazi katika mapato kwa kiwango gani? Je, tunajua wawekezaji hawa wakubwa akaunti zao ziko wapi? Tuna njia za kudhibiti kuhakikisha Taifa linapata gawio la haki na usawa? Je, mamlaka zenye dhamana ya kusimamia masuala haya zinatekeleza majukumu yao kikamilifu?

Tujenge nchi moja inayozingatia haki, usawa, amani, utengamao na unafuu wa kimaisha kwa kila mmoja huku kila mmoja akiwa na mazingira mazuri ya kutumia vipawa vyake kikamilifu kwa manufaaa yake mwenyewe na Taifa kwa ujumla. Tuna wajibu — kila mmoja wetu kuhakikisha tunafikia haya.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s