simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Fedha za Nje Zamwajibisha Waziri … Kashfa

leave a comment »

Rais Francois Hollande (kushoro) na waziri wa zamani Jerome Cahuzac (kulia)

Rais Francois Hollande (kushoro) na waziri wa zamani Jerome Cahuzac (kulia)

Waziri wa zamani wa Fedha wa Ufaransa Jerome Cahuzac ajitoa kwenye kinyang’anyiro

Waziri wa Fedha aliyejiuzulu kwa kashfa wa Ufaransa Jerome Cahuzac — alikutwa na kashfa ya kuwa na fedha kwenye akaunti ambayo hakuiweka wazi kwenye benki moja nchini Uswisi — ametangaza kwamba hatagombea kiti chake katika uchaguzi mdogo.

Aliliambia gazeti la Depeche du Midi kuwa alihofia kukumbwa na kampeni chafu zenye vurugu.

Bw Cahuzac — ambaye hapo kabla alijizolea sifa kama msemaji hodari dhidi ya uwekaji kwa njia haramu wa fedha katika benki za kigeni — alijiuzulu mwezi Machi.

Kashfa hiyo ilizidi kuharibu sifa ya serikali ya Rais Francois Hollande ambayo tayari ilikuwa imeshachafuka.

Bw Cahuzac ametozwa faini kwa kosa la kutolipa kodi.

Mwanzoni alikana taarifa zilizotolewa na tovuti ya habari za uchunguzi kwamba alimiliki akaunti ambayo hakuiweka wazi katika benki moja nchini Uswisi hadi 2010.

Lakini baada ya kukutana na mahakimu wa uchunguzi mwezi Aprili, alikiri kuwa na akaunti hiyo ambayo ilikuwa na kiasi cha euro 600,000 (zaidi ya Shilingi bilioni 1.2).

Aliliambia gazei la Depeche kwamba tayari amekwishahamishia fedha hizo nchini Ufaransa na kwamba atalipa madeni yake kwa dola na kukabidhi kiasi kitakachobaki kwa taasisi za hisani.

Chanzo: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

May 19, 2013 at 6:23 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: