simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mfalme Mpya … Tunajifunza Nini?

leave a comment »

Mfalme Willem-Alexander na Malkia Maxima wa Uholanzi

Mfalme Willem-Alexander na Malkia Maxima wa Uholanzi

Maelfu ya Waholanzi wakifuatilia tukio la kusimikwa kwa Mfalme Willem-Alexander

Maelfu ya Waholanzi wakifuatilia tukio la kusimikwa kwa Mfalme Willem-Alexander

Willem-Alexander ameapishwa kuwa Mfalme wa Uholanzi kufuatia kujivua madaraka kwa Malkia Beatrix, mama yake.

Anakuwa mfalme wa kwanza tangu mwaka 1890. Mama yake, 75, alitia saini kukubali kwake kujivua madaraka aliyoyashikilia kwa miaka 33.

Umati mkubwa uliovalia mavazi yenye rangi ya machungwa ulitawala jiji la Amsterdam ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria na kutoa heshima zao.

Mfalme mpya aliapa kuilinda katiba katika sherehe hizo zilizopambwa na kufana sana.”Ninaapa kulinda na kutunza uhuru na mipaka ya dola kwa nguvu zangu zote,” alisema Mfalme mpya.

“Nitalinda uhuru na haki za jumla na za kila mtu katika himaya yangu na nitatumia kila kilicho mikononi mwangu kwa mujibu wa sheria kuendeleza ustawi wa mtu mmojammoja na wa wote kama inavyostahili kufanywa na mfalme mwema … eeh Mungu unisaidie.”

Akiwa na umri wa miaka 46, mfalme huyu, ambaye mamlaka yake kisiasa yamepunguzwa sana, atalazimika kufanya kazi ya ziada ili kushawishi uwepo wa nafasi yake katika jamii.

Vijana wengi katika mitaa ya Amsterdam wanapata shida kuelewa lengo la kuwepo kwa familia ya kifalme — lakini wanapenda kusherehekea Siku ya Malkia.

Changamoto kubwa kwa Mfalme Willem-Alexander ni kuwaunganisha watu kwa ndani, kuwawakilisha kwa nje, na kuwajengea ari ya kufanya makubwa zaidi ili kuzidi kupanda juu.

Kwa upande wa mke wake, Maxima, ambaye sasa anakuwa malkia mpya, kuingia kwake kwenye ukoo wa kifalme wa Uholanzi kulikuwa na msisimko mkubwa.

Akiwa ni mzaliwa wa Amerika ya Kusini, familia yake ilichunguzwa kuona kama ilikuwa na uhusiano wowote na utawala wa kidikteta ulipata kutawala nchi yake ya asili — Argentina. Hata hivi, uchangamfu wake ulilichangamsha taifa.

Binti huyu wa ukoo wa kifalme alijitosa kwenye maji ya baridi na kuogelea huko Amsterdam: ilikuwa ni utayari wake wa kuyakabili maji hayo ya baridi sana ili kukusanya fedha za hisani kuwa jambo lililowavuta wengi miongoni mwa raia wa Kidachi.

“Amekuja na ameshinda,” anasema mwanahistoria wa Kidachi Henk te Velde.

“Ni muhimu aonyeshe kwamba anatambua nafasi yake — kuwa pembeni mwa mfalme na si malkia mkuu”, anasema mwanahistoria Han van Bree. Anaongeza kusema kwamba utayari wake kuzungumza na watu katika lugha yao baada ya kuolewa na Mwana mfalme Willem-Alexander, lilikuwa jambo lililopokelewa vema.

“Watu walivutiwa na ukweli kwamba mara baada ya kufika hapa, alianza mara moja kujifunza Kidachi,” anasema te Velder. “Tulivutiwa naye. Alionyesha kwamba anatuheshimu na anafanya jitihada kutuelewa”.

“Sasa hivi, ana uwezo hata wa kutaniana kwa Kidachi.”

Chanzo: BBC News

TUNAJIFUZA NINI?

– Wenzetu wanadumisha utamaduni wao, kitu kinachowaunganisha na kuwafanya wamoja kwa lengo la kuleta maendeleo ya wote.

– Kuna umuhimu wa kuheshimu misingi yetu ya asili inayotuunganisha, kutusaidia kuheshimu utu wa mtu, kutusaidia kusukuma maendeleo yetu sote, kutusaidia kukua zaidi kama binadamu, kuenzi na kuheshimu uhuru wa mtu mmojammoja kuwa vile wanavyotaka kuwa ili mradi hawavunji sheria, na misingi inayotusaidia kufikiri kwa usahihi na kisayansi

– Kutunza lugha zetu za asili na kuwafundisha wengine. Hii inahusu sana pia Lugha ya Kiswahili, tukienzi, tukitunze na tukieneze kwa jamii nyingine

– Tujifunze historia yetu ili kutusaidia kujua tunatoka wapi, wapi tulifanya makosa, tuyasahihishe vipi, na tufanye nini ili kufika kule tunakotaka kwenda

– Bila shaka nawe umejifunza mengi … unaweza kutushirikisha. Karibu.

Advertisements

Written by simbadeo

April 30, 2013 at 6:08 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: