simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dar … Ongeza Majina ya Vitongoji

with 2 comments

Mwanagati 1

Mwanagati 2

Mwanagati 3

Naam. Dar es Salaam ina vitongoji vingi. Kuna vile vilivyo maarufu kwa sababu ni vya miaka mingi, vingine kwa sababu ya aina ya watu wanaoishi huko, huku vingine vikiwa kwa sababu ya sifa na matukio yanayotokea huko. Hata hivyo, kuna vitongoji vingine ambavyo vinachipukia siku hizi … kwa kiasi kikubwa ni makazi mapya. Kadiri muda utakavyoruhusu tutakuwa tukivitembelea na kupata taswira chache.

Tuanze na Kitongoji cha Mwanagati. Barabara kuu ya kukufikisha Mwanagati ni ile inayoingilia Banana, kupitia Kipunguni na Kitunda. Alama kubwa ni Shule ya Sekondari Mzinga. Huko kuna eneo lililopimwa chini ya Mradi wa Viwanja 20,000. Kuna makazi yanayokuja juu kwa kasi na tayari kuna huduma nyingi muhimu.

Pia kuna barabara inayotokea Tandika. Hii lakini bado sijaipita.

Kwa ujumla mandhari hapa ni tambarare, udongo unaotawala ni kichanga. Kuna barabara za mitaa zilizowekwa wakati wa upimaji, na maji yanapatikana kwa kudrill ardhi wastani wa mita 60. Maji yanayopatikana ni baridi. Ni eneo ambalo nyakati za jioni, kuna mkondo wa upepo unaopita na bila shaka kwa wale wanaopenda utulivu … mbali na kelele za magari, huku watapapenda.

Hapo juu ni taswira chache zinazoonyesha mitaa ya kitongoji hicho.

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 30, 2013 at 5:25 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Asante sana kwa taswira hii na maombi ya wakazi wa Kitunda ni kuunganishwa na Tandika kupitia Mwanagati ili msongamano upungue katika eneo la Banana lakini mradi wa ujenzi wa daraja umeendelea kuwa kilio cha samaki baharini na hakuna anayaweza kuyaona machozi yake.Mipango ipo mezani kwa meya wa manispaa ya Ilala na kinachohitajika hapa na wananchi kuendelea kupaza kilio kupitia kwa waheshimiwa diwan wa Kitunda i na mbunge wa Ukonga.

  Like

  Ray E.Njau

  May 2, 2013 at 9:49 am

  • Naam Ndugu Ray. Maendeleo hayaji kwa urahisi, na pia watu wasichoke kusema … maana wao wakisema hata minazi iliyoko kule itasema … amini usiamini. Kudai haki inayolisukuma Taifa lote mbele ni haki ya kila mmoja.

   Like

   simbadeo

   May 2, 2013 at 10:10 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: