simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mifugo … Usafirishaji na Haki za Wanyama

leave a comment »

Jicho la kamera yetu lilinasa taswira hii jijini Dar es Salaam ... ng'ombe wakisafirishwa kutoka upande mmoja wa jiji kwenda mwingine.

Jicho la kamera yetu lilinasa taswira hii jijini Dar es Salaam … ng’ombe wakisafirishwa kutoka upande mmoja wa jiji kwenda mwingine.

Kilichovuta hisia ni namna ng’ombe hao walivyokuwa wameshonana. Tazama yule aliye mkono wa kulia, anayeeonekana kichwa tu. Ambebanwa kwelikweli na hana nafasi ya kunyajua kichwa zaidi, maana juu yake kuna kichwa cha mwingine. Fikiria amekuwa katika mkao huo kwa muda gani toka huko alikopakiwa hadi sasa, na toka wakati aliponaswa na kamera hadi huko alikokuwa akielekea!

Hata kama viumbe vingine haviongei, bado tunapaswa kujali kwamba navyo ni viumbe hai na huhisi maumivu na mateso. Kuna wataalamu wanaoshauri kwamba tuwatendee vema wanyama na mimea kwa sababu hawa baadaye — kwa njia ya kuliwa — huwa sehemu yetu wenyewe. Kuna wanaokwenda mbali zaidi na kusema kwamba namna unavyomtendea mnyama unayemwandaa kumchinja ina athari katika ubora wa nyama yake. Yule anayepitia mateso sana kabla ya kuchinjwa huwa na nyama ya ubora wa chini kuliko yule anayetendewa vizuri. Inasemekana kwamba kuna jamii hata huwawekea muziki wanyama wanaoandaliwa kuchinjwa ili wakati unapofika, basi wawe katika hali ya utulivu na hivyo kutoa nyama iliyo bora.

Tunapoheshimu viumbe wengine, tujaheshimu utu wetu. Viumbe vyote duniani tunategemeana sana. Inawezekana mara nyingi hatuoni ukweli huo, lakini … upo. Bila shaka ni kwa sababu hiyo kwamba vitabu vitakatifu vya imani mbalimbali huasa kuwa tuwatendee vema wanyama na viumbe vingine.

Pamoja sana

Advertisements

Written by simbadeo

April 29, 2013 at 12:51 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: