simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dar … Bila Maadili … Inatisha, Inaogofya

with one comment

Naam, yanaendelea kukwea juu, juu, juuuu...

Naam, yanaendelea kukwea juu, juu, juuuu…

Sio siri. Ukipita jirani yake au chini yake ... moyo unadunda ... maana aliyeumwa na nyoka, akiguswa na unyasi anaruka utadhani kawekewa spring ...

Sio siri. Ukipita jirani yake au chini yake … moyo unadunda … maana aliyeumwa na nyoka, akiguswa na unyasi anaruka utadhani kawekewa spring …

Yanachipuka kila kona. Sawa, kuna watu anapata ajira hapo na maisha yanakwenda. Kuna watu wataendesha maisha yao kwa kutegemea majengo hayo na maisha yatakwenda. Ni vitega uchumi vya uhakika. Ila matukio ya kuporomoka kwa majengo mahali mbalimbali duniani ikiwamo hapa Dar es Salaam … bado ni mabichi mno. Hapa Dar ndani ya mwezi mmoja uliopita watu zaidi ya 30 walipoteza maisha, Kule India karibu na mji wa Mumbai watu wapatao 70 walipoteza uhai, hivi majuzi hule nchini Bangladesh watu zaidi ya 350 wamepoteza maisha … yote ni kutokana na kuporomoka kwa majengo marefu.

Kwa hakika, wakati taarifa hizi zikiwa bado mbichi … kwa watu wengi … kila wapitapo chini ya majengo hayo yanayoendelea kurefuka miili huwasisimka. Na, bila shaka wapo wengi tu wanaochagua kutopita njia zilizo karibu na majengo hayo.

La muhimu, tuamini kwamba wale wenye jukumu la kusimamia ubora wa majengo wanafanya kazi yao sasa kwa umakini zaidi. Na wale wanaotakiwa kuwakagua hao wanaosimamia ubora, tunawasihi wakaze nati ili kwamba tuepuke majanga yanayoepukika. Jengo litakalokutwa limepungua ubora kidogo, lipigwe nyundo kabla halijaleta madhara.

Tukumbuke kwamba janga linapotokea sio tu kwamba kuna watu wanapoteza maisha, bali kuna wanaopata ulemavu wa kudumu na ule wa muda, kuna wanaopoteza mali lukuki, kuna wanaopoteza makazi, kuna wanaopoteza biashara, kuna kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi, kuna wanaopoteza wazazi na walezi.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, usimamizi wa ubora ukiwa wenye ufanisi, majengo hayo yanakuwa chachu muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmojammoja, taasisi na nchi kwa ujumla wake. Maana, kuna ofisi zitaendesha biashara zao humo, kuna huduma zitakazohitajika na watu watakaotumia jengo hilo, kuna mambo mengi yatakayochochea uchumi na mzunguko wa fedha. Kumbe, kuna watoto watakaokwenda shule kwa ajili ya majengo hayo n.k.

Yote inategemea kitu kimoja: UBORA. Na ubora hauwezi kupatikana pasipo na uadilifu na kufuata maadili.

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 29, 2013 at 10:30 pm

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. Hey there! I know this is kinda off topic however I’d figured I’d ask.
  Would you be interested in exchanging links
  or maybe guest authoring a blog article or vice-versa?
  My website goes over a lot of the same subjects as yours
  and I believe we could greatly benefit from each other.
  If you are interested feel free to shoot me an e-mail.

  I look forward to hearing from you! Superb blog by the way!

  Like

  world of tanks hack

  May 29, 2013 at 6:56 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: