simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Maji … Bajeti Inapotupwa Kapuni

leave a comment »

Huduma ya maji ni biashara kubwa maeneo ya mijini, hususani jijini Dar es Salaam. Tenki la ujazo wa lita 2,000 huuzwa kwa wastani wa Sh13,000. Kwa familia ya wastani wa watu 6 inahitaji walau kujaza mara nne kwa mwezi. Hiyo ina maana ya bajeti ya Sh52,000 kwa kaya hii. Kwa kipato cha Watanzania wengi, hiki ni kiasi kikubwa sana cha fedha, hasa ikilinganishwa na maeneo ambako huduma za maji za serikali zinafika, tofauti ya bei ni kubwa sana, maana huko kiasi hichohicho cha maji kinaweza kugharimu Sh16,000 kwa mwezi.

Huduma ya maji ni biashara kubwa maeneo ya mijini, hususani jijini Dar es Salaam. Tenki la ujazo wa lita 2,000 huuzwa kwa wastani wa Sh13,000. Kwa familia ya wastani wa watu 6 inahitaji walau kujaza mara nne kwa mwezi. Hiyo ina maana ya bajeti ya Sh52,000 kwa kaya hii. Kwa kipato cha Watanzania wengi, hiki ni kiasi kikubwa sana cha fedha, hasa ikilinganishwa na maeneo ambako huduma za maji za serikali zinafika, tofauti ya bei ni kubwa sana, maana huko kiasi hichohicho cha maji kinaweza kugharimu Sh16,000 kwa mwezi.

Kumbe basi, ni jambo la kutia moyo kwamba Wabunge wameacha tofauti ya itikadi zao na kusimamia uhalisia wa jambo — jitihada za dhati kwa upande wa serikali kuongeza ubora wa huduma ya maji, hususani upatikanaji wake kwa usawa na haki. Maisha hayawezi kwenda bila huduma ya maji. Mara nyingi haiingii akilini ni nini hasa kinachosababisha tusiweze kuvuna maji ya mvua kwa ufanisi. Ubora wa maisha utapatikana kwa kuongeza ubora wa huduma ya maji, kuyafanya yapatikane kwa gharama nafuu na katika eneo lililo karibu na wanapoishi watu. Kwa kuongeza ubora wa huduma hii, tutakuwa tukiongeza ubora wa huduma za afya na lishe, tutapunguza idadi ya watu wanaosumbuliwa na maradhi ya tumbo, kuhara na kuharisha na hata magonjwa ya ngozi, kwa maana hiyo, watu wengi zaidi watatumia muda wao kufanya shughuli za uzalishaji badala ya kuwa hospitalini/nyumbani wakijitibia.

Ni vema serikali ijipange upya na kuhakikisha kwamba inakuja na bajeti inayoendana na hali halisi ya mahitaji ya huduma hii nyeti kwa uhai wa watu na viumbe wengine. Ulinzi katika vyanzo vya maji lazima uimarishwe, iwekwe bayana kabisa kwamba kuharibu chanzo cha maji ni kosa la jinai na hatua za makusudi zichukuliwe kusimamia sheria hiyo. Viongozi wanaopokea rushwa ili kuwakingia kifua watu wanaoharibu mazingira na vyanzo vya maji waanikwe hadharani na sheria zichukue mkondo wake.

Mahali mbalimbali katika nchi yetu pamekuwa na taarifa za wafugaji kuvamia vyanzo vya maji ili kulisha na kunywesha mifugo yao. Pengine umefika wakati kwa nchi kufanya marekebisho katika sekta hii ya ufugaji — tuondokane na dhana ya kukumbatia wingi (idadi) mifugo na badala yake tugeukie kwenye ubora wa mifugo. Haina maana kwa kaya moja kumiliki ng’ombe 2,000 wakati ambapo rasilimali za kusaidia kuhimili idadi hiyo zinazidi kuwa haba. Ni akheri kwamba kaya hii ingesaidiwa kubaki na ng’ombe wasiozidi 50 lakini wenye ubora wa hali ya juu — kwa maana ya kutoa maziwa mengi, wanaohimili magonjwa mbalimbali na ambao mtu hahitaji kuhamahama huku na kule ili kuwatunza.

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 28, 2013 at 12:17 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: