simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Jamhuri ya Muungano ya Tanzania … Hongera ya Miaka 49

with one comment

M-degree ... maarufu ulio Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo wengi wamepita na kuonja kivuli chake ...

M-degree … maarufu ulio Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo wengi wamepita na kuonja kivuli chake …

Nkrumah Hall ... Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kina mijadala mingi sana imeendeshwa humu ... mingine ikihusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania ...

Nkrumah Hall … Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kina mijadala mingi sana imeendeshwa humu … mingine ikihusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania …

Leo Tanzania inasherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ni umri wa kutosha. Kama ni binadamu, basi ni umri wa mtu ambaye ana majukumu mazito katika kaya yake, kijiji chake, mtaa wake, ofisi yake, na hadi taifa. Pongezi nyingi kwa kila Mtanzania kwa kuchangia kwa namna moja ama nyingine kudumisha Muungano huu. Ikumbukwe kwamba hata wale wanaoukosoa Muungano huo nao wanachangia sana katika kuuimarisha — maana mti madhubuti lazima upigwe na upepo mkali, jua kali, mvua nzito, kiangazi kikali na pamoja na vyote hivyo na mti bado ukiendelea kuwapo pasipo kuanguka, basi vinachangia katika kuuimarisha.

Nimetumia picha za m-degree (mti maarufu pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Ukumbi wa Nkrumah, ambao nao upo katika mazingira ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama ishara ya baadhi ya vitu ambavyo kimyakimya vimekuwa na mchango madhubuti katika kudumisha Muungano wa Tanzania. Kuna Wazanzibari wengi na Watanganyika wengi ambao wamepita katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kupita kwao pale bila shaka kumechangiwa sana na kuwapo kwa Muungano huu ambao leo unatimiza miaka 49, yaani 50 kasoro mmoja.

Kuna mambo mengi yanayotuunganisha, ukiachilia mbali mkataba uliotiwa saini ili kuunga Muungano tarehe 26 Aprili, 1964. Baadhi ya mambo hayo ni mwingiliano wa watu wa Bara na Visiwani toka enzi za biashara ya utumwa na hata kabla ya hapo. Visiwa hivyo vimechota damu kutoka Bara na mbali zaidi ya bara, hadi sasa bado watu wanaendelea hata kuoleana — Bara na Visiwani kiasi kwamba watoto wanaozaliwa pamoja na wajukuu wengine ni wale ambao kote kote ni nyumbani, kuna miingiliano ya kibiashara, kiutamaduni, kiimani, kisiasa na hata kimtazamo katika fikra.

Muungano huu umesimama imara na ni ishara kuu kwamba Muungano wa Afrika kwa ujumla unawezekana. Tuna kila sababu za kuuendeleza, tuna kila sababu za kutafuta pale palipo na udhaifu na kuparekebisha, tuna kila sababu ya kuelekeza akili na juhudi zetu ili kuulinda kwa wivu mkali Muungano huu.

Hongera Watanzania, hongera Afrika. Tutazidi kuwaenzi mababa zetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume. Mwenyezi Mungu awajalie pumziko la milele huko mliko.

Heri ya siku ya Muungano kwa kila mmoja wetu!

Labda kwa wanalugha wanisaidie pia: Nyaraka nyiingi huonyesha ‘Jamhuri ya Muungano WA Tanzania’, lakini neno ‘Jamhuri’ linaqualify Tanzania, kwa nini isiwe ‘Jamhuri ya Muungano YA Tanzania’?

Pamoja sana.

Advertisements

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. I almost never create remarks, but after browsing through a few of the
  responses here Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Hongera ya Miaka
  49 | simbadeo2000. I actually do have a few questions for
  you if it’s okay. Is it just me or does it look as if like some of the responses look like they are coming from brain dead individuals? 😛 And, if you are writing on additional sites, I’d
  like to keep up with everything fresh you have to post. Could you post a list of the complete urls of your social networking
  pages like your twitter feed, Facebook page or linkedin profile?

  Like

  animefreak

  May 6, 2013 at 7:21 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: