simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Rais Agawa Fedha kwenye Gunia … Uganda

leave a comment »

Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Wachambuzi, wana-mitandao ya jamii wamkosoa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni aligawa hadharani gunia lililojaa fedha kiasi cha $100,000 (Sh160 milioni za Tanzania) kwa kikundi cha vijana, suala lililoibua mjadala kuhusu namna fedha hizo zitakavyotumiwa.

Tukio hilo la kutoa fedha za hisani lilitangazwa na kituo cha televisheni cha taifa, huku wachangiaji wengi kupitia mitandao ya kijamii wakilaani tendo hilo.

“Walau kulipaswa kuwekwe utaratibu mzuri ambao ungewafanya vijana watumie fedha hizo kwa namna yenye kuonyesha uwajibikaji,” alisema mchambuzi Peter Megelah.

Bw Museveni aliahidi kukisaidia kikundi hicho wakati wa kampeni zake mwaka 2011.

Pale Rais Museveni aliponyanyua gunia lililojaa Sh250 milion (kwa fedha za Uganda), alishangiliwa kwa kishindo, kisha alimkabidhi gunia hilo mwakilishi wa kundi la Busoga Youth Forum.

Katika tukio hilo pia alitoa zawadi ya basi dogo, lori moja na pikipiki 15, Kituo cha Televisheni cha NTV cha Uganda kilionyesha.

Mwakilishi wa BBC Catherine Byaruhanga jijini Kampala anasema Waganda wamezoea kumwona Rais wao akigawa fedha taslimu katika matukio ya hadhara.

Lakini kilichowashitua watu wengi safari hii ni kiasi cha fedha na ile taswira ya rais akiwa amebeba fuko lilotuna fedha.

Raia wengi wa Uganda wametoa maoni yao kupitia Twitter iliyokuwa na kiunganisho cha #sackofmoney.

Peter Magelah, mtafiti katika taasisi ya utafiti ya Acode aliiambia BBC: “Huu ni mchezo tu wa siasa wa rais kutaka kujipatia umaarufu.

“Je, tunajua jinsi gani fedha hizi zitatumika? Hakuna mfumo wa kuhakikisha uwajibikaji ili kwamba fedha hizi zipate kurudi baaday. Endapo vijana hawa watazitumia ovyo, basi ni nchi itakayokuwa imepoteza.”

Source: BBC News

Maoni

Kwa hakika kwangu ni tukio liliniacha nimepigwa bumbuwazi. Ni vema kusaidia vijana ili wapate kujikwamua na kusonga mbele na waweze kutoa mchango zaidi kwa maendeleo ya Taifa — lakini sina hakika kama hii ndio njia sahihi, hata kidogo. Kwa kiasi kikubwa ninafikiri kwamba amewaingiza mkenge vijana hawa, maana kuna watakaonufaika nazo sana (na hawa ni wachache), kuna watakaopata kidogo na kuna walio wengi watakaokosa kabisa. Tusishangae pia endapo tutasikia kuna watakaotoana meno na hata kuuwana kwa ajili ya kugombea fedha hizo.

Hii inanikumbusha michezo ya kwenye sinema pale mwizi (simaanishi kwamba Rais Yoweri Museveni ni mwizi au amepata fedha hizo kwa njia ya wizi, la hasha) anapokuwa ameiba fuko la fedha na katika harakati za kujiokoa, anachukua fedha kiasi na kisha kuzirusha hewani. Anapofanya hivyo, wale waliokuwa wakimkimbiza wanaacha kumwandama yeye na kuanza kutoana ngeu wakigombania fedha hizo zilizomwagwa chini.

Bado hii ni hadaa, nafikiri rais alishauriwa vibaya! Lakini pia huenda hii si dalili nzuri kwa kiongozi huyu, pengine sasa umri unamtupa mkono au amelewa mno madaraka kiasi cha kujigeuza kuwa kama wafalme wa zama za kale … Hii siyo tena hisani bali ni kujigeuza mungu-mtu na kwamba anaweza kutia mkono mfukoni na kuwamwagia fedha maskini.

Ni vema tuheshimu binadamu wenzetu na si kuwatendea namna hii. Tunashusha hadhi ya utu wetu na bara letu. Ndiyo maoni yangu.

Advertisements

Written by simbadeo

April 23, 2013 at 12:45 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: