simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Masika … Biashara na ya Mitaani

leave a comment »

Naam. Mvua inaponyesha Dar na katika viunga vyake, hali huwa tete.

Naam. Mvua inaponyesha Dar na katika viunga vyake, hali huwa tete.

Na ... usafiri wa aina hii wakati wa mvua ...

Na … usafiri wa aina hii wakati wa mvua …

Ndivyo hali huwa pale mvua inaponyesha jijini Dar. Shughuli nyingi husimama, miondoko ya watu hupungua. Hata hivyo, Waswahili husema, kufa kufaana … naam … ni wakati huu ambapo watu huona umuhimu wa kununua miamvuli. Lakini unaponunua mwamvuli wakati wa masika … ujue kuwa utalipa bei ya juu zaidi. Pichani hapo juu … mjasiriamali alibadili ghafla mwelekeo wa biashara yake na kuweka mtaji wake kwenye biashara ya miamvuli … bei ya kuanzia kwa mmoja ilikuwa Sh5,500 (wakati usio wa masika unaweza kuununua mwamvulia huo kwa Sh3,000 tu!) … naam … kufa kufaana!

Na usafiri wa pikipiki, almaarufu kama ‘bodaboda’ nao huwa kwenye wakati mgumu kipindi cha mvua. Dereva na abiria hulazimika kuweka kituo ili kupisha mvua ipite … maana matone ya mvua kwenye mwendo wa pikipiki huwa kama kugongwa na kokoto … fikiria maumivu yake. Wakati huohuo, macho hupata uoni hafifu na mvuke wa maji unaorushwa na magari huweka ukungu kwenye macho na hata miwani aliyovaa dereva wa pikipiki.

Lakini … huenda Wachina … au sisi wenyewe tutabuni mavazi ya kuwezesha mtu kusafiri kwa pikipiki hata wakati wa mvua … na mavazi hayo yatahusisha pia kuwa na helmet zenye miwani sahihi ambayo nayo itakuwa na ‘wipers’ … Tusubiri …

Advertisements

Written by simbadeo

April 22, 2013 at 2:48 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: