simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Chuki za Kidini … Watu 20 Wauwawa Nchini Burma

leave a comment »

Majengo yakiteketea kwa moto baada ya kuchomwa wakati wa machafuko kati ya Wabuda na Waislamu nchini Mynmmar (Burma)

Majengo yakiteketea kwa moto baada ya kuchomwa wakati wa machafuko kati ya Wabuda na Waislamu nchini Mynmmar (Burma)


Misikiti 5 yachomwa moto katika mapigano ya Wabuda na Waislamu

By: Associated Press
Source: Washington Post

MEIKHTILA, Myanmar — Kumekuwa na siku mbili mfululizo za machafuko kati wa wabuda (Buddhists) na Waislamu katikati mwa nchi ya Myanmar (zamani Burma) ambapo watu wapatao 20 wameripotiwa kuuwawa huku wakazi wa mji huo wakishindwa kufanya shughuli zao za kawaida mitaani, mwanasheria mmoja alisema siku ya Ijumaa.

Ijumaa asubuhi hakukuwa na dalili ya vurugu, lakini mji wa Meikhtila ulibaki katika hali ya taharuki na hatari, alisema Win Htein, mwanasheria kutoka chama cha upinzani cha National League for Democracy.

Makazi ya Waislamu yalitiwa moto na Wabuda wenye hasira walivizuia vikosi vya usalama kuuzima mot huo, alisema.

Walau misikiti mitano ilichomwa moto katika machafuko yaliyoanza Jumatano iliyopita, ikisimekana kwamba yalichochewa na mabishano kati ya sonara Mwislamu na wateja wake Wabuda. Katika machafuko hayo, mtawa wa Kibuda ni miongoni mwa waliouwawa kwanza, jambo lililokoleza mivutano na kusababisha genge la Wabuda kushambulia makazi ya Waislamu.

Mji wa Meikhtila ni takribani kilometa 550 kaskazini mwa jiji la Yangon, huku ukiwa na idadi ya watu 100,000, kati yao Waislamu wakiwa ni theluthi moja, alisema Win Htein said. Alieleza kwamba kabla ya machafuko hayo, mji huo ulikuwa na misikiti 17.

Ilikuwa vigumu kueleza kiasi cha hasara iliyopatikana katika mji huo kwa sababu wakazi walijawa na woga mno kiasi cha kushindwa kutoka nje na wapo waliokuwa wamekimbilia kwenye monasteri na maeneo mengine mbali na maeneo ya machafuko.

“Hatuko salama, hivi sasa tumekimbilia kwenye monasteeri,” alisema Sein Shwe, mwuza duka. “Hali ni tete na isiyotabirika.”

Migogoro ya kidini kati ya Wabuda (ambao ndio wengi) na Waislamu imedumu kwa miongo mingi nchini Myanmmar. Machafuko ya Meikhtila ni ya karibuni kabisa kufuatia yale yaliyohusisha Wabuda wa Rakine na Waislamu wa Rohingya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 200 na wengine 100,000 wakiwa hawana makazi.

Hii ni changamoto kubwa kwa serikali inayojaribu kuleta amani nchini na kujaribu kurejesha utawala wa kiraia kutoka kwenye mikono ya jeshi ili demokrasia itawale.

Wakati huohuo, BBC wameripoti kupokea video zilizoonyesha machafuko hayo. Katika video hiyo machafuko yaliendelea kwa watu kuuwawa, nyumba na misikiti na biashara kuchomwa moto na wanawake na watoto kuwa katika mahangaiko makubwa. Hata hivyo, wakati hayo yote yakiendelea, polisi walikuwa wakitama tu pasipo kuchukua hatua. BBC waliripoti kuwa hata baadhi ya video zilizopatikana zilipigwa na polisi hao.

Blogu hii inawaasa Watanzania kwa ujumla wao. Ni vema kila Mtanzania ahakikishe kwamba anakuwa na mchango ulio chanya katika kuendeleza amani nchini. Matukio ya hivi karibuni yanayohusishwa na haki ya kuchinja yamekuwa yakienda mbali kiasi cha kuanza kuwagawa. Tukumbuke kwamba pasipo kuwa na amani na utengemao hatuwezi kufanya shughuli za maendeleo.

Kujifunza hakuna mwisho. Hata kwa kushuhudia mambo mabaya yanayotokea katika nchi za wenzetu tunaweza kujifunza — kutopita njia hiyo. Tuchague daima njia ya kuiweka Tanzania na Watanzania mbele. Masilahi ya makundi yetu madogomadogo (kidini, kikabila n.k.) yasifunike masilahi ya Taifa zima. Tusimamie haki, uwajibikaji, uwazi, usawa na hutu — misingi waliyotuachia waasisi wa Taifa hili: Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 22, 2013 at 3:36 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: