simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Msako Boston … Mtuhumiwa Mmoja Auwawa

leave a comment »

Msako ukiendelea jijini Boston, Marekani. Picha ndogo ni ya mtuhumiwa anayesakwa.

Msako ukiendelea jijini Boston, Marekani. Picha ndogo ni ya mtuhumiwa anayesakwa.

Msako mkali Boston, Marekani

Sehemu kubwa ya jiji la Boston karibu hakuna kinachoendelea kwa sababu ya msako mkali dhidi ya mmoja wa ndugu wawili wanaotuhumiwa kutega na kulipua mabomu Mbio za Marathon za jiji hilo Jumatatu wiki hii.

Dzhokhar Tsarnaev, 19, ndiye anayeendelewa kusakwa baada ya kutoroka majibizano ya risasi ambapo kaka yake, mtuhumiwa mwingine, aliuwawa.

Polisi wanasema kuwa wamekwishakagua kati ya asilimia 60 hadi 70 ya eneo lililofungwa la kitongoji cha Boston.

Watu watatu waliuwawa na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa pale mabomu mawili yalipolipuka karibu na mstari wa kumalizia mbio za Marathon za siku hiyo ya Jumatatu.

Siku ya Ijumaa mchana, Ofisa Timothy Alben wa Idara ya Polisi ya Jimbo la Massachusetts alisema walikuwa “wakimsaka mtuhumiwa mlango kwa mlango, mtaa kwa mtaa” lakini taarifa za mahali alipo zilikuwa hazijapatikana.

Ndugu hawa, Dzhokhar na Tamerlan ni kina nani?

– Ni watoto wa wakimbizi wa jamii ya Chechnya katika eneo lenye mapigano la Caucasus, Kusini mwa Urusi
– Inaaminika familia yao ilihamia Marekani mwaka 2001, wakitokea Jamhuri ya Urusi ya Dagestan
– Waliishi katika mji wa Cambridge huko Massachusetts, mji ambamo ndimo kilipo Chuo Kikuu maarufu duniani cha Harvard
– Dzhokhar, 19, alitunukiwa fursa ya masomo ya juu; alitaka kusomea udaktari wa kupasua ubongo, kwa mujibu wa maelezo ya baba yake
– Tamerlan, 26, alikuwa ni mwanafunzi wa ndondi ambaye inasemekana alikatisha masomo yake ya chuo ili kwanza ajifue kwa ajili ya mashindano; alijieleza kama “mtu mwenye imani sana ya kidini” asiyetumia kilevi wala kuvuta.

Taarifa mpya zinasema mtuhumiwa anayesakwa anasadikiwa hivi sasa kuendesha gari la rangi ya Kijani, aina ya Honda.

Chanzo: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

April 19, 2013 at 10:01 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: