simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mlipuko Texas Marekani … Waua, Wajeruhi

leave a comment »

Mandhari ya mlipuko katika kiwanda cha mbolea karibu na mji wa Waco, Texas, Marekani

Mandhari ya mlipuko katika kiwanda cha mbolea karibu na mji wa Waco, Texas, Marekani

Mlipuko mkubwa kiwanda cha mbolea Texas waua, wajeruhi

Makumi ya watu wamejeruhiwa na idadi isiyofahamika kupoteza maisha baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika kiwanda cha mbolea karibu na mji wa Waco katika jimbo la Texas, nchini Marekani.

Dazeni kadhaa za majengo na makazi zimeharibiwa, na nyingine kushika moto, baada ya kiwanda cha West Fertilizer kulipuka majira ya saa 1.50 usiku kwa saa za Marekani, sawa na saa 6.50 usiku katika mstari wa Greenwich, sawa na saa 9.50 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Inaaminika kwamba kuna baadhi ya watu bado wamenasa kwenye majengo na idadi kadhaa ya askari wa zimamoto hawajulikani walipo.

Ofisa mmoja amethibitisha kwamba kuna watu wamepoteza maisha, lakini hakuweza kutaja idadi.

“Ilikuwa kama kujikuta uko kwenye kimbunga kikali. Kila kitu kilikuwa kinarushwa huku na huko. Ilikuwa kana kwamba dunia nzima ilikuwa ikitikiswa kwa nguvu,” alisema Debby Marak, shuhuda.

Dean Wilson, kutoka Idara ya Usalama wa Umma ya Texas, aliwaeleza waandishi wa habari kwamba walikuwa wakiendelea kutafuta watu kutoka nyumba hadi nyumba.

Alisema kwamba moto ulikuwa ukiendelea kuwaka kwa kasi kubwa na kwamba hakuna askari wa zimamoto waliokuwa wakijishughulisha kuuzima kwa sababu ya kuwepo kwa hatari ya milipuko zaidi.

Nusu ya wakaazi wa mji huo (wa watu wapatao 3,000) wamehamishiwa mahali salama, aliongeza kusema.

Gazeti la The Waco Tribune-Herald liliripoti kwamba kuna askari wa zimamoto waliokuwa wakijaribu kuzima moto katika kiwanda hicho wakati mlipuko ulipotokea, na kwamba baadhi yao walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa.

Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya milipuko inayosadikiwa kuwa ya kigaidi huko Boston, Marekani, katika mashindano ya mbio za Marathon za Boston. Watu watatu walipoteza maisha na zaidi ya 100 wengine kujeruhiwa. Upelelezi bado unaendelea.

Chanzo cha habari na picha: BBC News

Blogu hii inawapa pole nyingi wale wote waliojeruhiwa katika mlipuko huu na ile ya Boston. Vilevile inaungana na familia za waliopoteza jamaa zao katika misiba hii ya mfululizo. Pia inawaombea wale wote waliopoteza maisha ili wajaaliwe pumziko la amani na la milele.

Advertisements

Written by simbadeo

April 18, 2013 at 10:25 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: