simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mazao ya Misitu … Uhalali U Wapi?

leave a comment »

Lori lililosheheni magogo kama lilivyokutwa huko mitaa ya Mbagala.

Lori lililosheheni magogo kama lilivyokutwa huko mitaa ya Mbagala.

Tanzania inazidi kupoteza uoto wake wa asili kwa kasi kubwa sana. Kumekuwa na matumizi makubwa mno ya mazao ya misitu kuliko kasi ya kuotesha upya uoto huo. Tukiendelea na kasi hii kwa miaka mingine hamsini, si ajabu kwamba sehemu kubwa ya nchi itabaki jangwa. Tunaelewa umuhimu wa uoto wa asili, ikiwemo misitu, katika kutunza mazingira, kurekebisha hali ya hewa na kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi. Pengine swali kubwa hapa ni kwamba, je, wale tuliowapa mamlaka ya kusimamia na kutunza uoto wa asili na vyanzo vya maji, wanafanya hivyo kwa uadilifu?

Swali lingine linazaliwa. Matumizi haya makubwa ya mazao ya misitu yanatokana na nini hasa? Je, kwa kutumia kiasi hicho tunachotumia, nchi inapata manufaa yapi? Mathalani, pale tunapotumia mazao hayo kutengeneza mkaa, nchi inapata manufaa gani ya moja kwa moja?

Nishati mbadala imezungumzwa sana. Lakini kuna juhudi zipi zinafanyika kuhakikisha kwamba nishati mbadala inawafikia hata watu wa kipato cha chini? Hadi sasa tunaona kuna mitungi ya gesi, lakini hizo bei zake! Ni kiama kwa Mtanzania mwenye kipato cha shilingi 100,000 kwa mwezi. Familia ya wastani inahitaji walau mtungi wa kilo 15 kwa mwezi, na huu unauzwa si chini ya Shilingi 60,000.

Hizi mbao kwa ajili ya fenicha na ujenzi! Ufike wakati tuongeze ubunifu na kutumia mali ghafi nyingine. Kwa mfano, kwa nini tusiongeze matumizi ya chuma na madini ya fedha au hata shaba?!

Tafakari ni ndefu … endelea!

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 16, 2013 at 9:10 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: