simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kichaka Kariakoo … Hadi Watu Wakabwe?

with one comment

Naam. Ni palipokuwa na nyumba za Shirika la Reli ...

Naam. Ni palipokuwa na nyumba za Shirika la Reli …

Na ambapo palisemekana pangejengwa kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi ...

Na ambapo palisemekana pangejengwa kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi …

Huwezi kuamini kwamba hapa ni katikati kabisa ya jiji la Dar. Kichaka kinakua kwa kasi. Uzio uliojengwa kuzunguka eneo hilo unazidi kuporomoka. Unaweza kukisia nini kitafuatia … kama si eneo hili kugeuka maficho ya vibaka na wahalifu wengine. Matukio ya ukabaji yatakapoongezeka jirani na eneo hilo pia tusishangae, maana mazingira yanajitengeneza. Hivi kufanya usafi na kurudishia uzio huo vinagharimu kiasi gani? Kwa nini wasiwekwe watu wa kufanya usafi saa zote kuzuia kichaka kujitengeneza? Kwa nini wasiwepo walinzi ambao licha ya kuimarisha ulinzi, lakini watatoa taarifa mara moja pale sehemu ya uzio inapoanguka?

Hili ni janga … kama si kwa mtu mmoja mmoja watakaokabwa hapo basi kwa sehemu kubwa ya umma. Tujue kwamba wanawake, watoto na wenye ulemavu wapo hatarini zaidi kuwa wahanga wa eneo hili kama litaachwa liendelee kuwa hivi. Mamlaka zinazohusika zichukue hatua sasa!

Advertisements

Written by simbadeo

April 15, 2013 at 10:35 am

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. najiuliza kila wakati, hivi viongozi wanaenda kila wakati huko nchi za walioendelea hawaoni mipangilio ya miji yao? maduka kwa mstari saafi, barabara, maua, chemchemi za kutengeneza n.k, kwa nini hawaleti na huku hizo idea? takataka za kariakoo jamani hivi kodi za soko zinaenda wapi? kwa nini uongozi usiweke sheria na kufuatilia kila mwenye duka awe na pipa la taka na kisha zizolewe kwa wakati, kinyume cha hapo faini . Mungu ibariki Tanzania

    Like

    jennifer

    April 15, 2013 at 1:01 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: