simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwalimu Nyerere Professorial Chair … Africa’s 50 Years of Independence

leave a comment »

Venue: University of Dar es Salaam, Main Campus

Venue: University of Dar es Salaam, Main Campus

Fatma Almas Nyangasa of ITV and her team were there as well ...

Fatma Almas Nyangasa of ITV and her team were there as well …

Fully packed ... inside Nkrumah Hall at UDSM

Fully packed … inside Nkrumah Hall at UDSM

Nkrumah Hall ... outside

Nkrumah Hall … outside

Many more following the discussions from outside ...

Many more following the discussions from outside …

Jenerali Ulimwengu ... chairman of discussions on final day ...

Jenerali Ulimwengu … chairman of discussions on final day …

Discussions on top of discussions ... Azimio la Arusha limekufa?

Discussions on top of discussions … Azimio la Arusha limekufa?

And ... memories of the event must be captured in the form of photographs ... Time to pick one of two ...

And … memories of the event must be captured in the form of photographs … Time to pick one of two …

Mijadala ilikuwa mizito. Katika siku ya mwisho kuna mjadala ulijikita kwenye Azimio la Arusha la 1967. Lakini pia huwezi kuzungumzia Azimio la Arusha siku hizi pasipo kujadili kidogo kuhusu Azimio la Zanzibar la 1991.

Zitto Kabwe (Mb) alikumbusha kwamba Azimio la Arusha liliweka misingi muhimu ya taifa na hasa ikijikita kwenye miiko ya uongozi ikiwa ni pamoja na kuweka dira ya jumla ya maendeleo ya Taifa. Alisema kwamba Azimio la Zanzibar lilikuja kuondosha miiko hiyo na matokeo yake ni nchi kupoteza dira na viongozi kujineemesha wao na kusahau wajibu wao kwa nchi na wananchi.

Mzee Kingunge Ngombare Mwiru alieleza kwamba Azimio la Arusha halikuuwawa na Azimio la Zanzibar na kwamba miiko ya uongozi haikuondolewa, badala yake ilihamishiwa kwenye Katiba ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 18. Changamoto, anasema Mzee Kingunge, iko kwenye usimamiaji … nani anasimamia? Hakuna anayesimamia.

Wachangiaji waliongea mengi na hasa wakitaka nchi irudi kwenye Azimio la Arusha ili kurekebisha hali ya mambo. Viongozi watimize wajibu wao kikamilifu. Maendeleo yalenge watu kwani mapambano bado yanaendelea. Ilielezwa kwamba ni muhimu Watanzania wajifunze kikamilifu kuhusu Azimio la Arusha na yale yote yaliyoazimiwa kutekelezwa ndani yake. Kila Mtanzania ‘asambaze virusi vya Azimio’ kwani mapambano bado yanaendelea. Tanzania haitaendelea pasipo kufuata misingi iliyoainishwa kwenye Azimio la Arusha.

Ilisisitizwa pia kwamba Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 izingatiwe kikamilifu. Utaratibu wa Mipango ya Maendeleo Yanayopimwa kila baada ya Miaka Mitano itekelezwe na kusimamiwa. Mpango wa kwanza wa 2010 umekuja kwa kuchelewa sana. Huu ulipaswa uwe Mpango wa Tatu wa maendeleo.

Changamoto hapo ni kwamba hata sera ya ubinafsishaji ilitekelezwa huku kukiwa hakuna Mpango wa Maendeleo ambao ungesaidia kutathmini mafanikio ya sera hiyo. Kwa sababu ya mambo kupelekwa kinyemela, ubinafsishaji umekosa tija kwa Taifa ambapo viwanda vilivyo vingi vilivyobinafsishwa vimeshindwa kutoa mchango wa maana kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Wito ulitolewa kwa vijana kujifunza kwa dhati Azimio la Arusha, kutotegemea sana nafasi za kuteuliwa bali wajitume ili wapate kuchaguliwa kwa nafasi mbalimbali. Kila mmoja ahamasike kueneza ‘virusi vya Azimio la Arusha’.

Hamasa miongoni mwa washiriki ilikuwa juu. Mtazamo wa jumla ni kwamba kila mmoja ana wajibu wa kurekebisha hali ya mambo ambapo Taifa limekwenda kombo. Mifano iliyotolewa ni pamoja na kuzidi kupotea kwa misingi ya kujali utu wa mtu, matukio ya mauwaji yamekuwa yakiongezeka, watu wachache wanatumia madaraka waliyopewa kujineemesha wao na watu wao wa karibu huku Taifa likizidi kudidimia.

Kauli mbiu ya mijadala ilikuwa ‘Maendeleo ni Mapambano’, hivyo, mapambano bado yanaendelea, aluta continua!

Pamoja sana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: