simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Korea Kaskazini … Na Vitisho vya Vita

leave a comment »

Vikosi vya Korea Kaskazini katika gwaride. Je, taifa hili linatafuta nini linapotaka kuzipiga vita Korea Kusini na Marekani? Vita hivyo inavyovitafuta, vina tija gani kwa wananchi wake?

Vikosi vya Korea Kaskazini katika gwaride. Je, taifa hili linatafuta nini linapotaka kuzipiga vita Korea Kusini na Marekani? Vita hivyo inavyovitafuta, vina tija gani kwa wananchi wake?

KOREA KASKAZINI NA VITISHO VYA VITA

Korea (kwa ujumla wake) iliwahi kukaliwa na Vikosi Shirika baada ya Vita Vikuu vya Pili na hivyo kukomesha ukandamizaji uliofanywa na Japan.

Majeshi ya Kisovieti yaliikalia Korea Kaskazini na yale ya Marekani Korea Kusini, na kwa sababu nchi hizo shirika baadaye ziligeuka kuwa mahasimu katika Vita Baridi, mazungumzo ya kuziunganisha nchi hizo mbili yalishindikana na hivyo kuibua utawala tofauti kwa kila upande — Kaskazini na Kusini.

Katika Vita vya Korea vya mwaka 1950, Taifa la China lililokuwa la Kikomunisti chini ya uongozi wa Mao liliunga mkono Korea Kaskazini, wakati huo huo Marekani ilisaidia Korea Kusini ikihofia isije kugeuka na kuwa ya Kikomunisti.

Usitishaji wa mapigano wa mwaka 1953 ulirejesha amani, lakini ambayo ilikuwa tete, huku hali katika mpaka unaozigawa nchi hizo mbili ukiwa wenye migogoro ambayo imeendelea kudumu hadi leo.

Wadadisi wa mambo wamekuwa wakihoji kuhusu vitisho vinavyotolewa na Korea Kaskazini kuzishambulia Marekani na Korea ya Kusini, hata ikibidi kwa mabomu ya kinyuklia. Kuna maswali mengi:

— Korea Kaskazini inatafuta nini kupitia vitisho vyake hivi?
— Taifa hili lililoamua kuchukua mwelekeo wa kujitenga na ulimwengu, limeghadhabishwa na nini hadi kuamua kwamba sasa litaingia vitani?
— Iwapo vita vitaibuka kweli, je, Korea Kaskazini itanufaika vipi?
— Inawezekana yote haya ni kukosa tu unyenyekevu wa kuendana na yale jumuiya ya kimataifa inataka taifa hilo lifanye?
— Korea Kaskazini itapata hasara gani kama itaamua kuachana na vitisho hivyo na kuendana na mataifa mengine ulimwenguni?

Maswali ni mengi na hakika hayana majibu bado. Dunia yetu ina changamoto nyingi sana: vita, biashara za dawa za kulevya, biashara za binadamu, kukosekana kwa usawa katika maendeleo ya watu, utawala mbovu, umaskini, magonjwa, kukosekana kwa huduma bora za jamii, njaa, biashara ya silaha, uhamiaji haramu, mipasuko kwa sababu za kidini, kiitikadi, kirangi n.k. Ingekuwa vema sana kama viongozi wa Taifa la Korea Kaskazini wataachana na azma yao ya kuleta vita vingine. Vita hivyo havitakuwa na tija kwa taifa hilo na kwa mengine duniani. Ni vema waepushe matatizo yanayotokana na vita kwa watu wao wenyewe na wale wa kutoka mataifa mengine. Hakuna dhambi katika kuwa wanyenyekevu, japo kidogo. Ni sawa kuwa na misimamo na mitazamo inayojitegemea, lakini si katika mazingira yanayohatarisha usalama, amani na utulivu duniani.

Pamoja sana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: