simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Media Day … Siku ya Vyombo ya Habari

leave a comment »

Wadau wakuu wa vyombo vya habari ni wasomaji, watazamaji na wafuatiliaji wa habari ...

Wadau wakuu wa vyombo vya habari ni wasomaji, watazamaji na wafuatiliaji wa habari …

Blogu hii inaungana na wadau wote wa vyombo vya habari ulimwenguni kumtakia kila mmoja heri ya siku ya Vyombo vya Habari. Kwa hakika ni siku muhimu ambapo wanahabari wanakumbushana, kukumbusha na kujikumbusha kuhusu umuhimu wa sekta hiyo katika maendeleo na mustakabali wa maisha ya watu duniani.

Imesemwa mara nyingi kwamba vyombo vya habari ni sawa na pillar ya nne katika dola, kwa maana baada ya Bunge, Serikali na Mahakama, ule unaofuata ni Vyombo vya Habari katika ujumla wao. Sifa hii itakuwa na mashiko tu pale vyombo hivyo vitakapofanya kazi zao kwa kuzingatia kanuni na maadili yanayofanya pillar iwe pillar.

– kutoa habari pasipo upendeleo
– kutoa habari zilizotafitiwa vizuri
– kusimama katika UKWELI
– kusimimia HAKI na USAWA
– kutambua kwamba wajibu wa vyombo vya habari ni kuchochea FIKRA sahihi ili watu wafanye ‘informed choices’ ambazo kwazo watawajibika
– kuchochea UWAZI katika jamii
– kusaidia kuleta DIALOGUE baina ya pande zinazopingana

Kwa kuzingatia hayo na mengine mengi kama itakavyoelezwa katika siku hii, vyombo vya habari vitakuwa vikitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya watu, na hasa katika safari ya kukua kijamii, kiuchumi, kiroho na kiakili.

Pamoja na hayo, blogu hii inaungana na vyombo vingine vya habari pamoja na wadau wao ili kuwakumbuka waandishi wa habari wa Tanzania ambao kwa sababu ya kazi yao walipoteza maisha, kujeruhiwa au kupata misukosuko ya aina nyingine. Hapa tunakumbuka Daud Mwangosi aliyedaiwa kuuwawa mikononi mwa polisi mwezi Septemba mwaka jana, Bw Absalom Kibanda aliyetekwa na kuteswa na watu wasiojulikana wiki chache zilizopita, mwandishi wa habari aliyekutwa ameuwawa kule Kigoma, na mwandishi wa habari aliyeuwawa kule Mwanza.

Kwa ujumla, wahenga wetu walisema, ‘mjumbe hauwawi’, inasikitisha inapoonekana ‘wajumbe hawa, yaani waandishi’ wakiuwawa au kuteswa’ kwa namna moja ama nyingine, hususan katika Taifa ambalo kwa miongo kadhaa limejua amani, utulivu na maelewano, Tanzania. Matukio hayo kwa hakika yamepaka alama ya damu kwenye ramani ya nchi hii.

Blogu inatoa wito kwamba hatua za kuhakikisha haki za hao waliopoteza maisha ama kudhuriwa zinapatikana na wale waliofanya vitendo hivyo vya jinai wanachukuliwa hatua zinazostahiki.

Pamoja sana!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: