simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ghorofa Laporomoka … Ni Mumbai, India

leave a comment »

Ndugu, jamaa, mashuhuda na mtoto aliyeokolewa kutoka kwenye janga hilo ... huzuni imetanda.

Ndugu, jamaa, mashuhuda na mtoto aliyeokolewa kutoka kwenye janga hilo … huzuni imetanda.

Eneo la tukio, umati ukifuatilia kazi ya uokoaji inayoendelea.

Eneo la tukio, umati ukifuatilia kazi ya uokoaji inayoendelea.

Harakati za uokoaji zikiendelea ... kuondoa kifusi ... kila kinachoweza kutumika kinafanya kazi.

Harakati za uokoaji zikiendelea … kuondoa kifusi … kila kinachoweza kutumika kinafanya kazi.

GHOROFA LAPOROMOKA INDIA

Mashuhuda walisema jengo hilo liliporomoka “kama karata zilizokuwa zimepangwa wima moja juu ya nyingine”, anaripoti Rajini Vaidyanathan

Walau watu 40 wameripotiwa kupoteza maisha, wakiwemo watoto 11, baada ya jengo lililokuwa likiendelea kujengwa kuporomoka karibu na jiji la kibiashara la Mumbai nchini India, polisi nchini humo wameripoti. Dazeni kadhaa nyingine wameumizwa huku wengine wakihofiwa kunaswa katika jengo hilo lililokuwa na orofa saba katika mji wa Thane.

Polisi walisema jengo hilo lilikuwa likijengwa kinyume cha sheria na kwamba ujenzi ulikuwa ukiendelea huku baadhi ya orofa zikiwa tayari na wakazi ndani yake. Kuporomoka kwa majengo kunakotokana na ujenzi usiozingatia kanuni na taratibu, ni jambo linaloshutumiwa sana.

Mwandishi wa habari wa BBC, Sameer Hashmi, aliyekuwa katika eneo la tukio alisema waokoaji walikuwa wakiendelea na kazi ya kuondoa kifusi cha jengo hilo.

Janga hili limeibua ukosefu wa udhibiti katika ujenzi wa majengo nchini Inida. Polise wanasema mjenzi alitumia vifaa duni vya ujenzi na hakuwa na vibali vilivyomruhusu kujenga. Kuna mamia ya ujenzi haramu yanayoendelea katika jiji la Mumbai. Kwa sababu ya kasi ya ongezeko la watu, daima kumekuwa na mahitaji makubwa ya nyumba za gharama nafuu. Nyumba duni huuzwa kwa bei nafuu zaidi kuliko zile zilizojengwwa kwa kuzingatia vigezo vyote.

Wanaharakati wanatuhumu kwamba wajenzi hawa wenye tamaa ya utajiri wa harakaharaka hutoa rushwa kubwa kwa mamlaka zinazohusika ili wafumbie macho majengo haya haramu na huwa hawachukuliwi hatua zozote za kisheria. Wengi ya wale waliokuwa tayari wamehamia kwenye jengo hilo ni wale wa kipato cha chini hadi cha kati.

Mashuhuda walisema kwamba ujenzi wa jengo hilo ulianza yapata wiki sita zilizopita na kwamba hadi ajali inatokea, jengo hilo lililojengwa kwa kasi kubwa, tayari lilikuwa limeshafikia orofa ya saba na ile ya nane ilikuwa mbioni kukamilika. Hata kabla ujenzi haujakamilika kabisa, tayari wapangaji waliruhusiwa kuhamia na kushika orofa nne kati ya zile saba.

Chanzo: BBS World News kupitia mtandao

ANGALIZO

Tukio hili linakuja wiki moja tu baada ya jengo la orofa 16 kuporomoka jijini Dar es Salaam. Yapata watu 30 walipoteza maisha. Hapa nchini na kule India — matukio hayo hayakuwa ya kwanza. Yamejirudia mara kadhaa. Sababu za kuporomoka, ingawa uchunguzi bado unaendelea, kwa kiasi kikubwa ni kukosena kwa udhibiti wa kutosha ili kuhakikisha kwamba viwango vya ujenzi vinazingatiwa kikamilifu. Kama ilivyoripotiwa huko nchini India, tatizo la rushwa pia linajitokeza. Rushwa ni kama kansa. Inapoingia mwilini, mwili unapoteza mwelekeo wake wa asili wa ukuaji, vivyo hivyo kwa taifa linaloanza kupenywa na kansa ya rushwa. Dunia hivi sasa inazidi kufunguka. Katika uingizaji wa mambo nchini … ni muhimu kuhakikisha tunachuja sana. Kuna matatizo yanayotokea katika mataifa mengine, hayo ni vema kuyachuja na kuyaacha huko huko. Tuchukue tu yaliyo mazuri.

Blogu hii kwa mara nyingine inatoa pole kwa wafiwa wa matukio yote mawili — lile la hapa nchini na la huko nje.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: