simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Usalama Ulimwenguni … na Mustakabali wa Taifa

leave a comment »

Ramani kuhusu hali ya usalama wa mtu binafsi unaposafiri katika nchi mbalimbali duniani. Je, Tanzania tuko salama kiasi gani? Wewe na mimi tuna wajibu gani katika hili

Ramani kuhusu hali ya usalama wa mtu binafsi unaposafiri katika nchi mbalimbali duniani. Je, Tanzania tuko salama kiasi gani? Wewe na mimi tuna wajibu gani katika hili

HALI YA USALAMA ULIMWENGUNI

Taarifa za vitendo vya vikatili vya ubakaji watalii wageni nchini India na Brazil katika miezi ya hivi karibuni imetikisa tasnia ya safari za kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonukuliwa na chombo cha habari cha The Atlantic, idadi ya wageni wanaoitembelea India imeshuka kwa asilimia 25 tangu tukio lile la mwenzi Desemba la kubakwa mande kwa msichana mmoja kwenye basi katika mji mkuu wa New Delhi, ambapo anguko hilo linahusisha asilimia 35 ya wasafiri wanawake. Takwimu hizo zilikusanywa kabla ya tarehe 16 Machi, ambapo mwanamke mmoja raia wa Uswisi aliyekuwa akitembelea endo la katikati mwa India, Jimbo la Madhya Pradesh, kwa baiskeli akiwa na mume wake alibakwa mande na kundi la watu wapatao nane.

Katika jimbo hili, kuna wastani wa matukio tisa ya ubakaji yanayoripotiwa kila siku, kwa mujibu wa gazeti la the Washington Post.

Nchini Brazil, wakati ambapo mwanamke Mmarekani alipobakwa na watu watatu kwa muda wa saa sita Jumatatu, taarifa za ubakaji zimepanda kwa asilimia 150 tangu 2009, gazeti la The Atlantic liliripoti.

Kwa hiyo, si jambo la kushangaza kwamba Brazil na India zimekuwa ni baadhi ya sehemu za hatari zaidi kutembelea, kwa mujibu wa ramani iliyotayarishwa nchini Kanada na Idara ya Mambo ya Nje.

Lakini nchi hizo, siyo za hatari zaidi kabisa: Korea ya Kaskazini, Syria, Iraq, Iran, Afghanistan, Mali, Niger, Sudan, Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati and Somalia ndizo hasa nchi ambazo watalii wanaonywa “kuepuka kuzitembelea kwa sababu yoyote ile”.

Kwa nchi nyingine, kama vile Libya, wageni wanaonywa “kuepuka kwenda huko pasipo kuwa na sababu ya lazima”.

Rangi inayoonyesha hatari kwenye ramani hiyo pia inatoa maonyo kwa kulingana na eneo na wakati. Nchini Pakistani, watalii wanaonywa kuepuka: – maeneo zinakoripotiwa taarifa za harakati za kijeshi; – maeneo yote ya mipakani, isipokuwa eneo la mpaka la Wagha ambapo ni la kuvukia; – Mkoa wa Kashmir, ikiwa ni pamoja na Azad Kashmir; – Jimbo la Baluchistan, ikiwa ni pamoja na jiji la Quetta; n.k.

Nchini Mexico, wale “wanaotakiwa kusafiri hadi Monterrey, katika Jimbo la Nuevo León, wanaonywa kutotembea mara baada ya giza kuingia, na wanatakiwa kubaki katika kitongoji cha San Pedro Garza García.”

Kwa hiyo, je, ni nchi zipi ambazo ni salama kuzitembelea? Australia, Botswana, Canada, Chile, sehemu kubwa ya Ulaya, Greenland, Iceland, New Zealand, Malaysia, South Korea, Marekani na Uruguay, kwa mujibu wa taasisi
hiyo.

“Popote unapotaka kwenda duniani,” tovuti ya idara hiyo inashauri, “hakikisha unasoma taarifa za ushauri kuhusu kusafiri kwenda kwenye maeneo hayo, soma mara mbili: wakati unapopanga safari yako na muda mfupi kabla hujaanza safari. … Uamuzi wa kusafiri ama kutosafiri ni wajibu wa msafiri pekee.”

TAFAKARI

PENGINE ni muhimu kufuatilia taarifa za namna hii. Kama ramani inavyoonyesha, Tanzania tuna nafasi nzuri zaidi kuliko mataifa mengine ya Afrika ya Mashariki. Lakini, hili lisitufanye tubweteke.

Matukio ya hivi karibuni — hususani yale yanayohusishwa na ‘udini’ wa kuchinja nyama na kuingilia uhuru wa kuabudu wa wengine, siasa za kukabiliana na polisi, wizi, mauaji ya albino, migogoro ya ardhi, wizi, ukabaji, ujambazi na mengine kama hayo, yanaweza kabisa kutusukuma na kuingia kwenye ‘danger zone’. Ni rahisi sana kuporomoka kuliko kupanda.

Kila raia wa nchi hii na hasa viongozi sote kabisa tunawajibika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa ‘kweli nchi ya amani na utulivu na usalama’ kwa wenyeji na wageni. Tusahau tofauti zetu zote, tuiweke Tanzania mbele.

Tanzania imekuwepo na inapaswa kuendelea kuwepo daima.
Pamoja sana.

Taarifa hii ni kutoka Yahoo!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: