simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Wanawake … Itakuwa Vipi?

with 3 comments

Katika moja ya mitaa ya jiji la Nairobi, Kenya ...

Katika moja ya mitaa ya jiji la Nairobi, Kenya …

Endapo idadi ya wanawake duniani itakuwa kubwa zaidi kuliko ile ya wanaume? Fungua macho. Yafikiche kidogo, tazama mtaani. Unaona nini? Je, katika kila watu 10 unaona wanawake wangapi? Unaona wanaume wangapi? Je, katika kila watoto 10 wanaozaliwa, wa kike ni wangapi? Je, wa kiume nao?

Kwa hakika, kuna trend fulani inayotokea miaka hii. Huenda ndivyo Mwenyezi Mungu alivyopanga. Huenda ni mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwamba sasa hata wanawake nao wanatoka zaidi kwenda kwenye mihangaiko. Inawezekana ni mabadiliko ya kimaumbile kuhusu suala zima la utungaji mimba.

Vyovyote ilivyo, inafaa kustaajabia uzuri wa ulimwengu. Vile ulivyo umekamilika — uwe wa jinsia hii au ile. Huna sababu ya kujishuku na hata kutamani kuhamia jinsia nyingine. Why? Jipokee vile ulivyo kwani pamoja na jinsia yako kuwa hiyo uliyomo, bado unaweza kutoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya watu. Napenda zaidi neno ‘watu’ kuliko ‘binadamu’. Labda kwa sababu ‘watu’ ni ‘Kibantu’ na ‘bin-adam’ ni kutoka asili nyingine tofauti na ya ukanda wetu huu?

Well, pengine nilichotaka kusema ni kwamba kwa kufungua tu macho na kutazama eneo fulani, tunaweza kuibua fikra za kila aina? Nafurahi kuona watu hapa kwenye taswira hii wakitembea kwa amani. Kumbe basi, tuchague amani. Tuchague utulivu. Tuchague mapatano. Tuchague maelewano. Kila mmoja ana mchango mkubwa kwa watu wenzake.

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

April 2, 2013 at 10:18 pm

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , , ,

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Hiyo trend ndio hasa kinachoendesha ulimwengu tulio nao, kutokana na idadi yao kuongezeka, pili kukaribiana “50 to 50” elimu, uchumi, maamuzi, mtindo wa maisha, haki zao kuongezeka, nguvu za kisheria, wanakoelekea baada kuvuka kidogo tu (50-50). Vizazi vichache vijavyo kutakuwa na mahusiano ya mikataba, mostly men will be the “LOSER” na taratibu mwanaume atanyang’anywa nguvu yake ya utawala, kwa maana nyingine kutakuwa na single parent, sio kwa sababu ya wajane tu bali kwa mikataba mibovu tutakayo ingia katika jinsia hizi mbili,

  Like

  Jemedari Kalundi

  April 3, 2013 at 10:08 am

 2. Reblogged this on Jemedari Kalundi's Weblog and commented:
  Tafakari

  Like

  jemedarikalundi

  April 3, 2013 at 10:10 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: