simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dar na Maghorofa … Lipi Litafuatia Kuporomoka?

leave a comment »

Kuna majengo mengi mapya hapo ...

Kuna majengo mengi mapya hapo …

Sawa ... panapendeza machoni ... Lakini ni majengo yepi hapa ni majanga yanayosubiri kutokea?

Sawa … panapendeza machoni … Lakini ni majengo yepi hapa ni majanga yanayosubiri kutokea?

Naam. Leo habari iliyolishtua jiji ni inayohusu kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Ni tukio la kushtua kwa sababu nyingi.

Mosi. Matukio ya majengo kuporomoka yameshatokea katika jiji hili. Ilitarajiwa kwamba wenye dhamana ya kusimamia viwango vya majengo, hususani majengo marefu wawe wamefanya kazi yao vizuri ili matukio kama hayo yasijirudie, lakini kumbe sivyo.

Pili. Watu wana wasiwasi, idadi iliyosemekana kuathiriwa na janga hilo ni kubwa — kwa mujibu wa taarifa za awali kulikuwa na watu zaidi ya 60 — hivyo, wenye jamaa zao walioenda mjini kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za ujenzi, hivi sasa wana mashaka mengi.

Tatu. Tunarudi kwenye ubora. Mwekezaji anawezaje kumudu kujenga jengo lenye orofa 16 kisha ashindwe kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vya ubora?

Nne. Je, zile sifuri tulizoona hivi karibuni katika matokeo ya Kidato cha Nne ya 2012 … yanaweza kuwa just a tip of an iceberg? Maana yake nini? Wataalamu wanaoandaliwa na mifumo yetu ya elimu — wakandarasi, washauri, na wengineo — je, ni ambao somehow walifeli kwenye masomo yao ya taaluma zao?

Tano. Katika mlolongo wa uwajibikaji … nani ajitwike mzigo huu? Maana ni lazima watu wawajibishwe, au wawajibike wenyewe, au siyo?

Kuna mengi ya kuendelea kuandika … pengine haya yanatosha kwa sasa!

Wapumzike kwa amani watakaokutwa wamepoteza maisha katika janga hili ambalo kimsingi kabisa lingeweza kuepukwa!

Advertisements

Written by simbadeo

March 29, 2013 at 1:13 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: