simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Zaidi ya 25% ya Wanafunzi wa Kike Afrika ya Kusini Wanaishi na VVU

leave a comment »

Zaidi ya asilimia 25 ya wanafunzi wa kike nchini Afrika ya Kusini wanaishi na VVU kwa sababu ya kushiriki ngono na 'mashuga dadi'

Zaidi ya asilimia 25 ya wanafunzi wa kike nchini Afrika ya Kusini wanaishi na VVU kwa sababu ya kushiriki ngono na ‘mashuga dadi’

Afrika ya Kusini: ‘Zaidi ya 25% ya wasichana wanafunzi wanaishi na VVU’

Karibu 28% ya wanafunzi wa kike nchini Afrika ya Kusini wanaishi na VVU ikilinganishwa na 4% ya wavulana kwa sababu “mashuga dadi” wamekuwa wakiwatumia, Waziri wa Afya Aaron Motsoaledi alisema.

Waziri alieleza kwamba kiasi cha wasichana wanafunzi 94,000 pia walibeba mimba mwaka 2011 na 77,000 walitoa mimba katika suhula za umma, gazeti la The Sowetan liliripoti. Kiasi cha 10% cha watu wa Afrika ya Kusini wanaishi na VVU, takwimu rasmi zinaonyesha. Bw Motsoaledi amepongezwa sana kwa jitihada zake za kukabiliana na janga hili.

“Sasa ni wazi kwamba si vijana wetu wadogo wanaolala na wasichana hawa,” alisema Aaron Motsoaledi, Waziri wa Afya. Afrika ya Kusini imeendesha mradi mkubwa kuliko yote duniani ya kugawa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) tangu Rais Jacob Zuma alipomteua waziri huyo kusimamia wizara ya afya mwaka 2009.

Idadi ya watu wanaoishi na VVU wanaopokea ARV imeongezeka karibu mara mbili kutoka 678,500 hadi milioni 1.5 tangu alipoingia kwenye madaraka hayo, takwimu rasmi zinaonyesha.

‘Wanawaharibu watoto’

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Carolina katika jimbo la Mpumalanga, Bw Motsoaledi alisema idadi kubwa ya wasichana wanaoishi na VVU “inaumiza moyo wangu”.
“Sasa ni wazi kwamba wanaolala na wasichana hawa siyo vijana wetu wadogo. Ni watu wazima,” alinukuliwa na gazeti la The Sowetan akisema.
“Ni lazima tuwashughulikie hawa ‘mashuga dadi’ kwa sababu wanawaharibu watoto wetu.”
Bw Motsoaledi alisema watoto waja wazito wenye umri kati ya miaka 10 hadi 14, pia walikutwa na VVU.

Chanzo: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

March 14, 2013 at 3:25 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: