simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

“HABEMUS PAPAM FRANCISCUM”… TUMEMPATA PAPA FRANSISKO!

with 2 comments

Moshi mweupe kutoka dohani ya Kikanisa cha Sistine!

Moshi mweupe kutoka dohani ya Kikanisa cha Sistine!

Ni Papa Francis I aliyekuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, Argentina, Amerika ya Kusini ... Alijulikana kwa jina la Kardinali Jorge Mario Bergoglio

Ni Papa Francis I aliyekuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, Argentina, Amerika ya Kusini … Alijulikana kwa jina la Kardinali Jorge Mario Bergoglio

Amechagua jina la Papa Francis. Kanisa Katoliki lina watakatifu wawili waliotumia jina hili. Fransisko wa Assisi — aliyekuwa mtu wa watu wanyonge na mpigania imani. Yupo pia Fransisko Xavier aliyekuwa mmisionari mkubwa na ambaye alisaidia sana katika kuanzishwa kwa shirika la Wayesuiti. Ni kutoka katika shirika hili — ambalo hula kiapo maalumu kwa Baba Mtakatifu — kwamba Papa Francis I anatoka.

Ni mwanashirika la Jesuits. Ni mpenda wanyonge. Ni mtu mwenye misimamo madhubuti kuhusu imani. Katika uchaguzi wa papa wa mwaka 2005, alishika nafasi ya pili baada ya Papa Mstaafu Benedikto XVI.

Ni papa wa kwanza miaka zaidi ya 1300 kutoka nje ya Ulaya. Hata hivyo, ana asili ya Italia. Alipojitokeza kwa mara ya kwanza hadharani mara baada ya uchaguzi aliwasalimu watu: ‘Buona Sera’, ambayo ni salamu ya Kiitaliano ikiwa na maana ya ‘Habari za Jioni’.

Tofauti na mtangulizi wake, yeye si mtu wa kisomi zaidi bali ni mtu wa kuwa kati ya watu. Hata alipopanda ngazi katika nafasi za Kanisa, yeye alichagua kuishi maisha ya kawaida katika eneo la watu wa kawaida. Yaani hakuishi katika makazi maalumu ya Askofu Mkuu kule Buenos Aires.

Kwa uchaguzi wa jina, bila shaka atajaribu kulirejesha Kanisa katika mikono ya watu wa kawaida, wanyonge, ili kwamba liwe chombo cha kuwapa sauti kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Atakuwa na jukumu la kuwaunganisha watu ili kujiletea maendeleo na kuamua mustakabali wao.

Papa Francis I ametuomba tumwombee. Basi tufanye hivyo ili kwamba kwa nafasi yake ulimwengu upate kuwa mahali bora zaidi, pa haki na maelewano.

Pamoja sana. Pongezi kwa wote.

Advertisements

Written by simbadeo

March 13, 2013 at 11:42 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Tunakushukuru Ee Mwenyezi Mungu kwa tendo hili takatifu na kuwafunulia wale viongozi wetu waliokuwa wakimtafuta kiongozi wa juu wa kanisa ,Wewe ndiye uliyetaka awe huyu aliechaguliwa, tunakuomba umuongoze katika kazi yake hii mpya ya kuwachunga na kuwaongoza wakatoliki wote katika njia yenye kustahiki,,AMINA……………….HONGERA KWA WAKATOLIKI WOTE DUNIANI KWA KUMPATA MCHUNGAJI MWEMA.

  Like

  Andrew Msunga

  March 14, 2013 at 12:36 am

  • Tuombe awe na ujasiri wa kukemea maovu pasipo woga. Dunia ya leo imekuwa ikiendeshwa na wababe. Karibu kila jamii ina wababe wake. Hawa hawaheshimu sheria wala kanuni za kiutu. Ni muhimu kutafuta namna gani tunakuwa na sauti moja ili kufanya dunia hii iwe mahali bora zaidi pa kuishi. Nafasi ya upapa in mchango wa pekee katika kuleta usawa ulimwenguni. Pamoja sana.

   Like

   simbadeo

   March 14, 2013 at 2:58 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: