simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uhuru wa Habari: Vyombo vya habari Mali Vyagoma … Mhariri Akamatwa

leave a comment »

Magazeti yakiuzwa kwenye mitaa ya jiji la Bamako, Mali

Magazeti yakiuzwa kwenye mitaa ya jiji la Bamako, Mali

Mhariri huyo ni Boukary Daou

Vyombo vya habari vya binafsi vimeanzisha mgomo kufuatia kukamatwa kwa mhariri aliyechapisha barua iliyoeleza hali duni za kimaisha zinazowakabili askari wanaopigana dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu upande wa kaskazini. Mhariri wa Le Republicain, Boukary Daou, alikamatwa Jumatano iliyopita na alikuwa bado kufunguliwa mashtaka.

Askari walieleza hali yao kwamba hawana zana za kutosha za kivita na pia mgawo wa chakula ulikuwa duni — madai ambayo kwa kiasi fulani yanafanana na yale ya askari walioleta mapinduzi mwezi Machi mwaka jana nchini humo.Serikali ya mpito ya Mali haikutoa tamko kuhusiana na kukamatwa kwa mhariri huyo wala mgomo wa vyombo vya habari.

‘Kukosa uzalendo’

Mwandishi wa BBC Alex Duval Smith aliyeko jijini Bamako anasema jumla ya magazeti 40 tofautitofauti huchapishwa kila wiki nchini humo — na hakuna hata moja lililokuwa kwenye meza za kuuzia magazeti Jumanne asubuhi jana. Mapambano yanayotendelea kaskasini dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu yalianza mwezi Januari 2013 kwa msaada wa vikosi vya jeshi la Ufaransa. Katika mgomo huo, vituo 16 vya masafa mafupi ya redio ama vilikuwa kimya au vilikuwa vikipiga tu muziki, alisema mwandishi huyo.

Waziri wa Mawasiliano, Manga Dembele, alisema Bw Daou alitenda pasipo umakini wala kuzingatia uzalendo kuwa kuchapisha barua ya wazi ya askari hao kwenda kwa rais, hata hivyo, hakuna tamko rasmi la serikali kuhusiana na kesi hiyo.

Katika barua hiyo, askari pia walilalamika kuhusu maofisa wa ngazi za juu wa jeshi hilo waliokuwa wakiishi maisha ya anasa huko Bamako wakati wenzao wakiteseka katika mstari wa mbele wa mapambano. Kepteni Amadou Sanogo aliongoza mapinduzi ya mwezi Machi 2012 akidai kwamba jeshi halikuwa na vifaa vya kutosha kuweza kuwakabili vema wapiganaji wa Ki-Tuaregi huko kaskazini mwa Mali.

Hali ya uhuru wa kupashana habari inazidi kuwa tete katika Bara la Afrika, ambapo katika siku za karibuni kumekuwako matukio ya waandishi wa habari kukamatwa, kuuwawa au kushambuliwa kiasi cha kuwadhuru kimwili. Wiki moja iliyopita, Mhariri mwandamizi nchini Tanzania, Absolom Kibanda, alishambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake. Shambulizi hilo lilikuwa baya kiasi cha kumwathiri jicho, kucha, meno na vidole. Hivi sasa anaendelea na matibabu huko Afrika ya Kusini.

Nchini Somalia waandishi wa habari wamekuwa wakiuwawa kwa kushambuliwa kwa risasi, kutekwa nyara n.k.

Chanzo: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

March 12, 2013 at 6:00 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: