simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Breaking News! … Papa Benedikto XVI Kujiuzulu Mwezi Huu

with 3 comments

Pope Benedict XVI

Pope Benedict XVI

Pope says he will resign

The Pope is to resign at the end of this month in an entirely unexpected development, the Vatican has confirmed.

The 85-year-old became Pope Benedict XVI in April 2005 following the death of John Paul II.

The reasons behind the head of the Catholic Church’s surprise resignation have yet to emerge.

Resignations from the papacy are not unknown, but this is the first in the modern era, which has been marked by pontiffs dying while in office.

At 78, the former Cardinal Joseph Ratzinger was one of the oldest new popes in history when elected.

He took the helm as one of the fiercest storms the Catholic Church has faced in decades – the scandal of child sex abuse by priests – was breaking.

http://www.bbc.co.uk/news/world-21411304

Papa atangaza kujiuzulu

Baba Mtakatifu — kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani — atajiuzulu wadhifa wake huo mwisho wa mwezi huu, hatua ambayo haikutarajiwa hata kidogo, Vatikani imethibitisha.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85 alichaguliwa kuwa Papa na kuchukua jina la Benedikto XVI mwezi Aprili 2005 kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Papa Yohana Paulo II.

Sababu za uamuzi huu wa kushtukiza wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki lenye waumini zaidi ya bilioni moja duniani kote bado hazijawekwa bayana.

Kujiuzulu kutoka kwenye wadhifa wa papa si jambo geni katika historia ya Kanisa, hata hivyo huu utakuwa ni uamuzi wa kwanza wa aina yake katika karne za hivi karibuni, ambapo utaratibu uliozoeleka ulikuwa kwa mapapa kufariki wakiwa madarakani.

Katika umri wa miaka 78, Kardinali Joseph Ratzinger alikuwa ni miongoni wa watu wazee kabisa kuchaguliwa kwa wadhifa wa upapa katika historia.

Aliingia madarakani katika kipindi ambapo Kanisa lilikuwa likipitia kipindi kigumu sana kwenye historia yake — hasa mitikisiko ya karne kadhaa za kashfa za ngono na watoto zilizowakabili baadhi ya makasisi wake.

Chanzo: http://www.bbc.co.uk/news/world-21411304

Advertisements

Written by simbadeo

February 11, 2013 at 2:29 pm

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. MMMMMH,MIMI HADI SASA SIAMINI KAMA KWELI ATAJIUZULU,,HALAFU NINASHAUKU KUJUA SABABU YA HAYO YOTE,KIONGOZI WETU ANATUACHAJE WATU WAKE,YEYE AKIJIUZURU NDIO SULUHISHO YA MATATIZO?MMMMMHHH MIMI SIAMINI KABISA

  Like

  Andrew Msunga

  February 12, 2013 at 2:03 am

  • Ndugu Andrew Msunga

   Roho Mtakatifu anafanya kazi kila sekunde. Usihofu. Hekima iliyotumika kufikia uamuzi huu inazidi hekima za binadamu wa kawaida. Kikubwa ni kusali, kuombea amani na utulivu duniani na utazidi kuona kazi za Bwana Mungu. Uwe na imani. Usihofu. Tunaweza kutembea hata juu ya maji tukiwa na imani iliyo thabiti.

   Karibu sana.

   Like

   simbadeo

   February 12, 2013 at 5:12 pm

 2. Ni hekima ya ambayo ameitumia kulingana na afya yake,ambapo ameona bora aongoze mtu mwingine, ila sisi tunahiaji kumuomba mungu ashushe roho mtakaifu kumpata mrithi wake.

  Like

  Andrew Msunga

  February 14, 2013 at 1:37 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: