simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ufugaji Nyuki … Biashara, Sanaa, Utamaduni, Mazingira

leave a comment »

Ufugaji Nyuki unaweza kufanywa kwa minajiri ya biashara - chanzo cha mapato.

Ufugaji Nyuki unaweza kufanywa kwa minajiri ya biashara – chanzo cha mapato.

Ufugaji nyuki pia inaweza kuwa kazi ya sanaa na utamaduni, ambapo watu huweka ubunifu katika mitindo ya mizinga na mbinu za urinaji asali. Ni ujuzi adimu.

Ufugaji nyuki pia inaweza kuwa kazi ya sanaa na utamaduni, ambapo watu huweka ubunifu katika mitindo ya mizinga na mbinu za urinaji asali. Ni ujuzi adimu.

Vilevile ufugaji nyuki ni njia mojawapo muhimu ya kutunza mazingira na kuongeza bioanuwai. Nyuki huchavusha maua ili kuandaa mimea hiyo kuingia hatua nyingine muhimu katika ukuaji wake na utoaji matunda. Mahali penye nyuki wengi, watu hawawezi pia kwenda huko kuharibu mazingira ovyo ... wakithubutu, cha moto watakiona.

Vilevile ufugaji nyuki ni njia mojawapo muhimu ya kutunza mazingira na kuongeza bioanuwai. Nyuki huchavusha maua ili kuandaa mimea hiyo kuingia hatua nyingine muhimu katika ukuaji wake na utoaji matunda. Mahali penye nyuki wengi, watu hawawezi pia kwenda huko kuharibu mazingira ovyo … wakithubutu, cha moto watakiona.

Hii ni asilimia ndogo sana ya mizinga iliyo katika mazingira ya Maua Seminari. Kutokana na mizinga hiyo, taasisi hiyo inajipatia asali — ambacho ni chakula bora kwa afya, ni dawa na ni kiburudisho tosha. Elimu ya kujitegemea huanzia katika miradi ya aina hii katika ngazi ya taasisi. Kwa namna asali inavyopendwa duniani, sioni sababu kwa nini Tanzania isigeuke kuwa mzalishaji nambari moja wa zao hilo. Hebu fikiria endapo kila kijiji na taasisi zenye maeneo makubwa — relatively — zitakuwa na mradi wa ufugaji nyuki. Naamini tuna uwezo wa kuzalisha tani na tani za asali pamoja na mazao mengine yanayotokana na kazi hiyo. Mabadiliko yataletwa na SISI wenyewe. Kuna mengi bado ya kujifunza kutoka taasisi hii ya Maua. Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

January 8, 2013 at 11:14 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: