simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Krismas … Umuhimu wa Maeneo ya Wazi

leave a comment »

Kwa sababu ya ukosefu wa maeneo mwafaka ya wazi na burudani kwa watu wa rika zote ... nyakati za sikukuu kubwa kama Krismas, watoto humiminika maeneo kama Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar, na kando ya fukwe za bahari.

Kwa sababu ya ukosefu wa maeneo mwafaka ya wazi na burudani kwa watu wa rika zote … nyakati za sikukuu kubwa kama Krismas, watoto humiminika maeneo kama Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar, na kando ya fukwe za bahari.

Lakini pale uwanjani ... kuna point ambapo watoto hawakuruhusiwa kuingia ... japo wengi walitamani kufanya hivyo na maeneo waliyokuwemo hayakuandaliwa rasmi kwa ajili ya kundi kubwa la watu, ni maeneo ya kupita tu.

Lakini pale uwanjani … kuna point ambapo watoto hawakuruhusiwa kuingia … japo wengi walitamani kufanya hivyo na maeneo waliyokuwemo hayakuandaliwa rasmi kwa ajili ya kundi kubwa la watu, ni maeneo ya kupita tu.

Kwa hiyo, ni watu wazima wachache tu waliokuwa upande wa pili ... ambako watoto wengi walitamani kufika ... lakini walipigwa stop!

Kwa hiyo, ni watu wazima wachache tu waliokuwa upande wa pili … ambako watoto wengi walitamani kufika … lakini walipigwa stop!

Biashara nazo zilichachamaa ...

Biashara nazo zilichachamaa …

Kulikuwa na kuuza na kununua ... Je, wateja (watoto) walizingatia thamani ya nini wanakula? Not sure. Wao furaha yao ilikuwa uwezo wa fedha waliyokuwa nayo ... kwamba anatoa mia mbili anapata paketi ya ubuyu ... basi ilikuwa furaha kuu kwao.

Kulikuwa na kuuza na kununua … Je, wateja (watoto) walizingatia thamani ya nini wanakula? Not sure. Wao furaha yao ilikuwa uwezo wa fedha waliyokuwa nayo … kwamba anatoa mia mbili anapata paketi ya ubuyu … basi ilikuwa furaha kuu kwao.

Mababa wa mipango miji wana jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba kila baada ya umbali fulani, kunakuwa na eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya burudani — kwa watoto na watu wazima. Haya hayana budi kuwa maeneo ambayo watu wataingia bure au kwa ada ndogo. Maeneo ya recreation huongeza uwezo wa ubunifu na kuwafanya watu kutambua thamani ya mazingira yaliyopangiliwa vema. Ukosefu wa maeneo kama hayo ambamo familia zinaweza kukusanyika katika siku za sikukuu na kuburudika, kunalazimisha jamii kujitenga. Watoto wanazurura mchana hadi jioni. Watu wazima wanamiminika kwenye kumbi zao za starehe giza linapoingia. Mpangilio huu unafanya watu wazima wakose fursa ya kutambua na kuappreciate umuhimu wa kuwa na maeneo ya wazi wanapoweza kukaa na familia zao.

Utamaduni wa kujenga familia huhusisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na suhula muhimu za kutolea burudani kwa makundi makubwa makubwa. Pengine ingefaa kila mtaa katika jiji la Dar es Salaam liwe na eneo la namna hiyo ili watu wasilazimike kusafiri mbali sana kutafuta eneo la burudani. Burudani ni muhimu kwa ukuaji wa kiakili, kimaadili na hata kiafya na kisaikolojia, lakini ni muhimu kuwepo na maeneo maalumu kwa ajili hiyo. Ikibidi kuwahusisha wawekezaji, basi ifanyika hivyo. Dar es Salaam na miji mingine nchini inahitaji sana huduma hii.

Pamoja sana na boxing day njema.

Advertisements

Written by simbadeo

December 26, 2012 at 10:59 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: