simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Zuma Mshindi… Wapi Afrika ya Kusini Inakwenda?

leave a comment »

Jacob Zuma (kulia) alisema atafanya kila jitihada kulinda demokrasia

Jacob Zuma (kulia) alisema atafanya kila jitihada kulinda demokrasia

ANC yamchagua tena Jacob Zuma kama kiongozi wake

Jacob Zuma amechaguliwa upya kama kiongozi wa chama kikuu kinachotawala cha African National Congress.

Kwa mujibu wa habari za BBC, alipata ushindi wa kishindo katika kura karibu 4,000 zilizopigwa katika ukumbi wa chama hicho wa mikutano wa Mangaung.

Wakati huohuo mpinzania wake Kgalema Motlanthe nafasi yake ya umakamu wa rais imechukuliwa na mpinga ubaguzi wa rangi mkongwe Cyril Ramaphosa.

Bw Zuma alitarajiwa kushinda uchaguzi huo wa ndani wa chama dhidi ya mpinzaniwake aliyekuwa pia makamu wake, Bw Motlanthe.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 70 alishinda kura 2,986 kati ya 3,977.

“Tunaweza kujivuna kwamba sisi ni viongozi wa jamii yetu, tuna kitu cha kuchangia katika mfumo wa kidemokrasi wa nchi yetu, kwa Jamhuri hii ya Kidemokrasi ya Afrika ya Kusini,” alisema Bw Zuma baada ya kutangazwa mshindi.

Chama cha ANC kimetawala Afrika ya Kusini tangu kung’olewa kwa utawala wa wachache mwaka 1984, chama ambacho kinatarajiwa kushinda uchaguzi wa taifa wa mwaka 2014. Bw Zuma kwa hiyo bila shaka ataendelea kuwa rais hadi mwaka 2019.

Source: http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-20765678

MAONI:

Kwa maoni yangu, Zuma ni kiongozi mashuhuri na mwenye uwezo mkubwa wa kushawishi, hasa watu wa kawaida nchini mwake. Hiyo ni tunu ya pekee. Ila kwa muda aliokaa madarakani kama Rais amenonesha kwamba hiyo si nafasi inayomfaa. Yeye angebaki tu kama mtu wa kuunganisha umma ili kuleta umoja na maelewano. Naamini kazi hiyo angeifanya vema sana. Lakini hili la urais — ni viatu vikubwa sana kwake. Ni chini ya uongozi wake tumeshuhudia vitendo vilivyokuwa vikifanywa na serikali ya wachache — enzi za siasa ya ubaguzi wa rangi — vikijirudia: askari kuuwa watu wasio na silaha, watu wanaopigania haki zao. Kumbukumbu za wafanyakazi wa migodini waliouwawa bado zingali mbichi.

Swali linalotatiza hapa ni kwamba, imekuwaje wanachama wa ANC wamemchagua tena kwenye nafasi hiyo — tena kwa ushindi mnono? Hiyo ni pamoja na kwamba umri wake sasa unazidi kuyoyoma. Hivi sasa tayari ana umri uliotajwa kwenye Biblia kwamba ndiyo ‘stahili’ ya mtu — miaka 70. Endapo atachaguliwa tena kuwa Rais mwaka 2014 — ataongoza nchi yake hadi mwaka 2019! Wakati huo atakuwa anakaribia miaka 80!

Hivi, tuna nini sisi Afrika? Mbona tunaendekeza sana kurudia kuchagua viongozi wale wale kila kukicha wakati ambapo tunajua wazi kabisa kwamba hawana tena jipya la kutuletea? Tunatumiaje kura zetu? Afrika ya Kusini — nchi yenye uchumi mkubwa zaidi katika nchi za Kiafrika — inapaswa kuwa na kiongozi mwenye mwelekeo wa kimapinduzi, mapinduzi yatakayoiondolea nchi hiyo na bara zima utegemezi. Taifa hilo linahitaji kiongozi atakayekuwa na nguvu ya kukemea viongozi wenzake barani Afrika wanaoendeleza migawanyiko ya kikabila, kitabaka, rangi na wanaokubali kuwa watwana wa wamiliki wa multi-national corporations yanayonyonya rasimali za Afrika.

Muda aliotumikia Mzee Jacob Zuma kama kiongozi wa nchi yake ulikuwa unamtosha tayari. Hivi sasa ilikuwa wakati wa kuleta fikra mpya na mwelekeo mpya.

Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

December 19, 2012 at 7:30 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: