simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ujambazi Jijini Dar … Mtuhumiwa Mmoja Anaswa

leave a comment »

Suspect6Suspect4Suspect2Suspect5Suspect1Suspect3

Inasemekana kuna majambazi wanne waliokuwa wakifukuzia fedha zilizobebwa kwenye gari dogo lililokuwa likiendeshwa na mwanadada mmoja. Ilikuwa katika Barabara ya Nyerere eneo la Banda la Ngozi. Hapo ndipo songombingo ilipotokea. Wale wanaosadikiwa kuwa majambazi walitoa bastola na kumtisha yule mwanadada. Mwanadada aliwapa mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha hizo. Watu wengine walikuwa wakishuhudia kinachoendelea. Baada ya majambazi hao kunyakua fedha hizo, walianza kukimbia kwa pikipiki. Abiria mmoja kwenye moja ya daladala, inasemekana aliamua kuruka kutoka dirishani na kuwavaa wale majambazi.

Katika hekaheka hiyo, ndipo majambazi watatu yalitimua mbio kwa pikipiki. Mtuhumiwa mmoja alijaribu kukimbia kwa miguu … lakini hakufika mbali. Ndipo alipokamatwa na kuanza kupata kichapo hicho kabla askari huyo wa usalama barabarani hajaingilia kati kumnusuru na kupata nguvu kutoka kwa askari wengine waliofika muda mfupi baadaye.

Kwa kadiri ya maelezo wa mashuhuda, fedha zilipatikana.

Pengine inafaa kuzingatia sana suala la usalama. Inabidi watu wapunguze kutembea na kiasi kikubwa cha pesa. Pale inapobidi kufanya hivyo, ni vema kutumia njia zinazokubalika — kutumia vikosi vya jeshi la polisi au kampuni binafsi zinazofanya kazi hiyo kwa ulinzi wa kutosha.

Mwisho wa mwaka, viwango vya uhalifu huongezeka sana. Sababu yake ni nini? Tusaidiane kutafiti. Kila mmoja akae chonjo na kusaidia katika usalama.

Wakati blogu hii ikipongeza wale wote waliofanikisha kushindwa kwa tukio hilo la wizi, inatoa pia wito kwamba si vema kuchukua sheria mkononi. Kama kuna tukio, watuhumiwa wakamatwe na kisha taratibu za kisheria zifuate. Si kazi ya raia kuhukumu na kutoa haki, kuna chombo chenye jukumu hilo, nacho ni Mahakama.

Advertisements

Written by simbadeo

December 3, 2012 at 1:38 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: