simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwisho wa Mwaka … Majira Tatanishi

leave a comment »

Huku na kule unakopita kipindi hiki unakutana na miti hii al-maarufu kama Mikrismasi. Ni miti ambayo maua yake huchanua kipindi cha mwisho wa mwaka hadi mwanzoni mwa mwaka unaofuata. Ni kipindi cha machipuo mara baada ya jua kali sana la kiangazi na lililounguza majani na miti. Kijani kinatawala maeneo mengi kwani karibu sehemu kubwa ya nchi inakuwa ikipata mvua — kwa kiasi chake. Mandhari haya yanayotawala kipindi hiki huamsha hisia za matumaini, furaha na uchangamfu.

Lakini kuna utata. Katika kipindi hiki pia uhalifu huongezeka sana. Sina hakika kwa nini. Nafikiri ni vema wanasayansi ya jamii wafanye utafiti wa kina ili kubaini kwa nini hasa uhalifu huongezeka katika nyakati za mwisho wa mwaka. Naamini matokeo ya utafiti huo yatawafaidi si tu jeshi la polisi ili kubuni mbinu mpya, bali hata sisi raia ili tutazame tunajilinda vipi.

Kwa hayo machache … nimtakie kila mpenzi wa blogu hii na rafiki katika Facebook Mwisho wa mwaka mwema, mtulivu, wenye furaha na matumaini kwa mwaka mpya mwingine … Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

November 24, 2012 at 12:48 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: