simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Bosi wa BBC George Entwistle Ajiuzulu … ‘Tuhuma Hazikuwa na Ukweli’

leave a comment »Bw George Entwistle

Katika kile kinachoonekana kwamba dhoruba zinazoikabili BBC hazijatulia, Kiongozi Mkuu wa Taasisi hiyo ya habari ya nchini Uingereza, ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake ili kupisha uchunguzi makini zaidi kufanyika.

Aliwaambia waandishi wa habari: “When appointed to the role, with 23 years’ experience as a producer and leader at the BBC, I was confident the trustees had chosen the best candidate for the post, and the right person to tackle the challenges and opportunities ahead.

“However, the wholly exceptional events of the past few weeks have led me to conclude that the BBC should appoint a new leader.”

Akimaanisha kwamba: “Nilipoteuliwa kushika wadhifa huu, nikiwa na uzoefu wa miaka 23 kama prodyuza na kiongozi ndani ya BBC, nilikuwa na imani kwamba wadhamini walikuwa wamechagua mtu bora kabisa kwa nafasi hiyo, mtu sahihi wa kushughulikia changamoto na fursa zilizo mbele. Hata hivyo, matukio ya aina yake katika majuma ya hivi karibuni yameniaminisha kuhitimisha kwamba BBC haina budi kuteua kiongozi mpya.”

Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya BBC Lord Patten alisema: “As the editor-in-chief of that news organisation George has very honourably offered us his resignation because of the unacceptable mistakes – the unacceptable shoddy journalism – which has caused us so much controversy.

“He has behaved as editor with huge honour and courage and would that the rest of the world always behaved the same.”

Yaani: “Kama mhariri mkuu katika taasisi hiyo ya habari, George ameandika ili kujiuzulu wadhifa wake kwa heshima kwa sababu ya makosa yasiyokubalika — uandishi wa juujuu wa habari — ambao umesababisha migongano mikubwa. Ametenda kama mhariri mwenye heshima kubwa na ujasiri kwa namna ambayo ingalifaa sana ulimwengu mzima ungalikuwa ukitenda kama yeye.”

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni wa Uingereza Maria Miller alisema tukio hilo lilikuwa “a regrettable situation, but the right decision”. Ambapo kwa tafsiri ya haraka alisema: “kujiuzulu kwake lilikuwa tukio la kusikitisha lakini ambalo ni uamuzi sahihi.”

Kwa maoni yangu: Hapa tunaona dhana ya uwajibikaji inavyofanya kazi. Bwana George amejiwajibisha kwa makosa yaliyofanywa na watendaji wa chini yake. Heshima, hadhi na kuaminika kwa taasisi nzima kumetishiwa na makosa ya watu wachache. Kwa kuona hilo kiongozi mkuu ameamua kukaa kando kwa kujiuzulu. Hii ina maana kwamba atakapopatikana kiongozi mpya, utafanyika uchunguzi huru ili haki itendeke.

Mara nyingi sana mambo ya kimaadili yanapokwenda kombo katika jamii zetu barani Afrika, huwa tunakuwa wepesi sana kusema ‘Ah. Si vijana wanaiga mambo ya nje!’ Tukio hili na mengine mengi yanatufundisha kwamba, kuangamia kwa maadili katika jamii yetu SIYO lazima iwe kwa sababu ya tamaduni za Kimagahribi. Wenzetu bado wana fadhila wanazoendelea kuzishikilia sana: Uwajibikaji, kujituma, kujiaminisha kutokana na kuaminiwa, kusimamia ukweli na haki, kutopendelea n.k. Kwa hakika tunaweza kabisa kujifunza fadhila hizi na kuzifanyia kazi katika vyombo na taasisi zetu, kwenye vyama vyetu vya siasa, kwenye makampuni tunamofanyia kazi, kwenye jamii, dini na mijumuiko ya aina nyingine — ya kisheria na isiyo ya kisheria.

Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

November 11, 2012 at 12:11 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: