simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

South Dar Mbagala … Kazi ya Mikono ya Watu

leave a comment »

Workshop … Kazi zinaendelea. Gurudumu la maendeleo linasukumwa kwenda mbele.

Matunda. Yanasubiri kuvunwa.

Ndiyo. Mbagala inabadilika. Unaweza kuishi huko miezi sita bila kuwa na sababu ya kwenda mjini. Huduma zote unapata huko huko.

Na miundombinu inaimarishwa … hata kama ni kwa kusahihisha upungufu uliokuwepo mwanzo.

Benki zinashindana kutafuta wateja na kuwasogezea wateja huduma.

Vituo vya mafuta navyo vinashindana …

Ukiona namna hii … ujue shughuli huko mbele ni pevu.

Huduma za hospitali nazo hazikubaki nyuma. Usiniulize kama kuna madaktari na dawa na vifaa vingine … hilo sikulitafiti safari hii. Lakini wenyeji watatueleza na wenye dhamana na mamlaka nao wataibuka kutueleza.

Kwa ujumla, Mbagala inabadilika. Miongo miwili iliyopita, watu wengi wasingetamani kuishi Mbagala. Huduma zilikuwa duni sana na changamoto zilikuwa nyingi. Bado changamoto ni nyingi hata sasa, lakini kuna huduma nyingi, hasa za kibiashara zilizojisegeza karibu. Je, maisha ya watu yanakuwa bora zaidi … pengine hilo ni swali linalohitaji utafiti wa kina ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi takwimu nyingi sana. Kwa sasa uwanja huu hauna uwezo huo, ila pengine siku za usoni. Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

October 1, 2012 at 11:58 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: