simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

International Peace Day … Siku ya Kimataifa ya Amani

with one comment

Amani. Iwapi? Ina rangi gani? Ni kitu gani? Je, ni wakati gani mtu/jamii inakuwa na amani? Fedha zinapojaa mifukoni? Mmh! Hapana, maana nadhani Israeli wangekuwa na amani tele, maana wao mambo yao super. Unapokuwa na madaraka makubwa kabisa … mfano Rais? Mmh. Nayo hapana, mbana saa zote wamezungukwa na watu waliobeba silaha nzito nzito, ulinzi mkali. Kumbe basi amani inapatikana wapi? Amani ni nini? Ni nini? Amani inapatikana katika umri upi? Utotoni? Ujanani? Utu uzimani? Uzeeni? Ukikongweni?

Haya, jamani. Leo ni siku ya amani duniani. Ila bado tunaendelea kuisaka amani hiyo. Kuna wanaosema kwamba Tanzania ni kisima cha amani. Ni kweli? Inawezekana ndiyo. Inawezekana hapana. Hebu fikiria: Unafunga mlango pasipo kuwa makini. Unajibana kidole hadi kucha inatoka. Damu inatoka. Umebaki na kidonda. Kidole kinauma na kupwita kana kwamba kimejaa usaha. Je, kwa vile ni kidole ndicho kilichoumia basi viungo vingine vya mwili ule ule vinaendelea kubakin na amani na utulivu? Kweli? Hebu fikiria upya kuhusu mfano huo. Kama kuna wenye mabilioni katika taifa hilihili … bila kujali wameyapata vipi, na kama kuna watu hohehahe katika taifa hilihili … je, ni kundi lipi la watu lenye amani kwenye nafsi zao?
Amani. Wewe ni kitu gani? Unapatikana wapi? Tukutambue vipi? Ndugu yako Furaha yuko wapi? Pesa = Amani? Kama hivyo ndivyo, basi wale wanaofanya kazi BoT wana amani kubwa sana!

Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

September 20, 2012 at 11:03 pm

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , ,

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. mke akisema haitaji amani alafu unaishi naye ndani utamfanyaje?

    Like

    wandai

    February 2, 2014 at 10:56 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: