simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Sumbawanga … Kuna Kazi Inaendelea

with one comment

This slideshow requires JavaScript.

Ndiyo. Kuna kazi inaendelea kati ya mji wa Tunduma na ule wa Sumbawanga. Ni ujenzi wa madaraja na barabara kwa kiwango cha lami. Kipande hiki cha barabaraka kitakapokamilika kujengwa, kitapunguza sana umbali kati ya Mbeya na Sumbawanga, kwa maana hiyo pia kati ya Sumbawanga na Dar es Salaam. Kwa sasa inachukua takribani saa nane kusafiri kutoka Mbeya hadi Sumbawanga. Si ajabu muda huo utapungua kwa zaidi ya asilimia 50, yaani ichukue kati ya saa tatu hadi nne.

Haya ni maendeleo makubwa. Pengine lililo la muhimu ni kuhimiza ubora. Wanaosimamia wahakikishe kwamba barabara na madaraja hayo ni ya kudumu. Tusingependa kuona yale ambayo hutokea katika barabara nyingine kwamba hata kabla haijakabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika, zinakuwa tayari zimeanza kubomoka.

Katika taswira pia utapata sehemu ndogo ya mji wa Sumbawanga ambapo kuna double roads. Zilipojengwa hizo double roads zilisababisha kelele nyingi sana kuhusu viwango vya ubora wake. Baadaye naona kimya. Je, nini kiliendelea? Au zilizobomolewa na kujengwa upya? Kwa mwenye taarifa atufahamishe ili nasi wapita njia tupate kuelewa.

Pamoja sana Tanzania yetu!

Advertisements

Written by simbadeo

August 16, 2012 at 10:04 am

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. maendelea makubwa mno!!

    Like

    yasinta

    August 16, 2012 at 3:32 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: