simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tunduma … na Kasi ya Ukuaji

leave a comment »

This slideshow requires JavaScript.

Mji wa Tunduma ulio kwenye mpaka unaoziunganisha nchi za Tanzania na Zambia unakua kwa kasi kubwa kwelikweli. Kila mara ninapopita hapo, ninakuta mji umetanuka sana. Shughuli za kibiashara ni nyingi hasa kwa sababu ya mwingiliano wa watu wengi na hasa wasafirishaji, kwa maana ya madereva, wasaidizi wao na wafanyabiashara.

Pamoja na upande huu ulio chanya, Tunduma inakabiliwa na changamoto mbalimbali, mathalani:
1. Ukuaji wake haufuati mipango bora ya mji
2. Kuna uhaba mkubwa wa maji
3. Masuala ya usalama bado ni hafifu sana
4. Miundombinu kama barabara nazo bado ni finyu. Msululu wa malori yanayosubiri kuvuka mpaka kwa upande wa Tanzania yanaweza kufikia hadi urefu wa kilomita mbili au tatu. Hii ina maana wafanyabiashara na wasafirishaji wanapoteza muda mwingi sana hapa. Jambo hilo linawatia gharama zaidi kwani kama binadamu watakuwa na mahitaji anuai.
5. By inference: kuchelewa kwa msafirishaji kukaguliwa kunachochea rushwa kwa maana kwamba dereva au mwenye mzigo anayetaka kushughulikiwa haraka ukaguzi wa mzigo wake anaweza kumshawishi mtu anayehusika ili kwamba afanyiwe mambo yake chapu chapu.

Kwa haraka haraka, kwa ushauri, hizi ni changamoto ambazo zimo ndani ya uwezo wa serikali yetu. Miundombinu ipanuliwe, askari polisi waongezwe, vyanzo vipya vya maji vitafutwe na wataalamu wa mipango miji waingie Tunduma na kufanya kazi yao kwa umakini zaidi. Haya yakifanyika, kuna uwezekano wa kuufanya mji huu kuwa wa kisasa, kuwa kivutio cha utalii na kwa hiyo kufanya mchango wa mji kama mji kwa uchumi wa mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla kuongezeka mara nyingi sana. Nawasilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

August 15, 2012 at 12:35 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: