simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Jivanjee Garden … Nairobi

with 3 comments

Ni eneo tulivu katikati ya Jiji la Nairobi. Unapotaka kutafakari mambo yako, unapotaka kupumzisha akili baada ya siku ndefu yenye mambo mengi, unapotafuta mahali patulivu ili ujisomee kitabu au gazeti, unapotafuta mahali unapoweza kusikia mahubiri ya dini, unapotaka kupata mahali pa kuvuta sigara kwa uhuru pasipo kuvunja sheria (maana Nairobi huvuti sigara ovyo wala popote … ukithubutu kufanya hivyo … utayajua yaliyomtoa kanga manyoya) … Basi ingia kwenye bustani hizi za Jivanjee.

Maeneo kama haya ni muhimu sana katika jamii. Haipendezi kwamba kila mahali pawe pamejengwa majengo makubwa makubwa tu na hakuna mahali pa kupumzika. Pengine maeneo kama haya yaliypaswa kuwa mengi zaidi katika jiji lenye joto kama Dar es Salaam. Mnazi mmoja peke yake haitoshi … na bado haitoi fursa zilizopo Jivanjee. Wana mipango miji … mpoooo???

Advertisements

Written by simbadeo

August 10, 2012 at 12:40 am

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. mie nalia na usafi wa miji yetu kama hakuna usafi bustani itakaaje? itakuwandio dampo jingine, kama kuna mwanaharakari wa usafi nijulisheni tujiunge, yaani unanikera!

  Like

  jennifer

  August 10, 2012 at 10:10 am

 2. naua tukiamua tunaweza, tupate tu sapoti toka kwa wenye madaraka, UCHAFU JAMANI!

  Like

  jennifer

  August 10, 2012 at 10:11 am

  • Da Jennifer. Suala la usafi tumeligeuza siasa. Usafi huwa unafanyika pale kiongozi fulani anapotaka kuonekana kwenye vyombo vya habari basi atahamasisha usafi kwa siku hiyo lakini hakuna mwendelezo. Nadhani tuchukue jukumu mikononi mwetu … kila mzazi amfundishe mtoto kuuchukia uchafu wa kila aina kuanzia nyumbani, mitaani na katika mazingira mengine. Kila kaya ikifanya hivyo, naamini hali itabadilika na miaka kumi na tano kutokea sasa tutakuwa tukiishi, kufanya kazi na kutembea katika mazingira yaliyo safi. Asante kwa mchango wako wa mawazo.

   Like

   simbadeo

   August 11, 2012 at 1:12 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: