simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dar roads … Slowly but surely

with 3 comments

Upanuzi wa barabara ya Morogoro, husasani kutoka Kimara kuelekea mjini unaendelea. Kasi ni ya wastani. Kwa ujumla inaleta matumaini. Huenda itasaidia kidogo kupunguza foleni, ingawa ili kuondoa kabisa tatizo la foleni, itakuwa lazima kuongeza kasi. Lakini si kuongeza kasi tu bali kuongeza idadi ya barabara zinazopanuliwa na kuimarisha nyingine, hasa zile za mzunguko katika jiji la Dar kwa kuzijenga kwa kiwango cha lami.

Swali la uchokozi. Katika wakandarasi wote wazawa ilishindikana kupata kampuni ya kuchukua zabuni ya upanuzi huu? Vipi kuhusu zabuni-bia (joint venture) nayo ilishindikana? Ni wazo tu limepita kichwani. Cha msingi ni kwamba wataalamu wazawa tukaze buti ili kujijenga katika suala la ushindani. Hatuna budi kuweza kushindana na makampuni ya nje … tuzingatie kukuza ubora wa kazi zetu, umakini katika utendaji na usimamizi, uadilifu, kwenda na wakati na kila mara kufungua masikio ya nini kinaendelea katika nyanja za taaluma zetu. Tunaweza. Tujipange na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Advertisements

Written by simbadeo

August 7, 2012 at 12:23 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , ,

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. ubora wa kazi zetu, umakini katika utendaji na usimamizi, uadilifu, kwenda na wakati na kila mara kufungua masikio ya nini kinaendelea katika nyanja za taaluma zetu.Kaka Simba haya ndio mambo hatunayo na ndiyo maana wako nyuma. ukimpa tu tenda 50% matumizi yasiyo ya lazima na 35% ndio kazi na 15% unajua inakokwenda. tukiamua tunaweza.

  Like

  jennifer

  August 7, 2012 at 7:53 am

 2. Haraka haraka haina baraka

  Like

  yasinta/kapulya

  August 7, 2012 at 1:02 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: