simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mpunga … Mashine katika Mpanda

with 2 comments

Zao la mpunga limepanda chati sana katika Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi. Wafanyabiashara wa mazo ya humiminika kipindi cha mavuno ambapo hununua mpunga kwa bei ya chini na kisha kuhifadhi kwa ajili ya kipindi ambapo chakula kimeadimika. Wapo pia ambao husafirisha bidhaa za chakula hadi maeneo mengine ya nchi au hata nchi jirani. Vyovyote vile ilivyo, ni vema wenye uwezo wa kulima waongeze uzalishaji, wauze zaidi na kujiletea maendeleo. Ila wakulima pia wakumbuke kuweka akiba kwa ajili ya mahitaji yao kwa kipindi chote hadi mavuno yanayofuatia. Si busara kuuza mavuno yote na kisha kuhangaika wakati wa masika — kipindi ambacho chakula huwa haba.

Kwa upande mwingine, zao hili — kama yalivyo mengine ya chakula — lina tija zaidi kuliko zao la tumbaku. Binafsi nina ugomvi na zao hili. Ukiondoa suala la madhara ya kiafya, zao hili lina madhara makubwa sana kwenye mazingira. Kila ninapotembelea Mpanda, ninaona kwamba misitu inaanza kutoweka. Yote sababu ya zao la tumbaku. Harubu ya kazi ya tumbaku ni kubwa, kiasi ambacho sidhani kama kinalingana na kipato. Malipo kwa zao hili yamekuwa yakilalamikiwa sana kwamba yamejaa utapeli, udanganyifu na hata wizi wa kimachomacho. Kwa sababu hizi, binafsi nafikiri zao la tumbaku halina tija kwa wakazi wa Mpanda na vitongoji vyake — si sasa tu bali hasa kwa vizazi vijavyo ambavyo vitarithi ardhi iliyochoka na iliyo nusu jangwa.

Tumechelewa kufanya mabadiliko — huenda bado, lakini ni lazima kufanya uamuzi sasa.

Ni katika kijiji cha Ngomalusambo, Wilayani Mpanda, mashine ya kusaga. Sikupata muda wa kuhoji kuhusu usalama wa chombo hicho kufungwa hapo nje! Yeyote anayejua majibu kwa swali hili atushirikishe. Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

August 4, 2012 at 11:10 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. mpunga, mweeehh nimeulima huo wakati naishi Lundo na Kingole/Litumbandyosi ..kazi yake ni kungolea, kupandikiza na kuamia ndege

  Like

  yasinta/kapulya

  August 6, 2012 at 6:20 pm

  • Kipunga … ndiyo chenyewe … halafu kikiwa kile cha kulima mwenyewe … yaani ndiyo kunoga.

   Like

   simbadeo

   August 7, 2012 at 12:13 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: