simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tutembelee Shule ya Sekondari ya Mwese … Elimu

with 5 comments

Ni mara baada ya kipindi …
Sehemu ya ofisi ya walimu …
Kwenye Paredi …
Kwenye Paredi …
Kwenye Paredi …
Kaimu Mwalimu Mkuu …
Mwalimu Massawe akitoa maelezo kuhusu mfumo wa umeme unaotumia nishati ya jua …

Kwa nini Shule ya Sekondari ya Mwese inapaswa kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya kitaifa:
– Idadi ya wanafunzi madarasani ni ndogo 
– Idadi ya walimu kulinganisha na mahitaji, karibu kuna uwiano 
– Fursa ya kujisomea katika saa za ziada ipo, hata usiku kwani shule ina nishati ya umeme wa jua 
– Mazingira ni tulivu na hakuna bugudha nyingi za watu na magari 
– Hali ya hewa ya mwese ni nzuri, ni hali ya baridi ya wastani 
– Hali ya chakula Mwese ni ya kuridhisha 

Changamoto – Wanahitajika walimu zaidi 
– Wazazi hawana budi kuamka na kujali elimu ya watoto wao kwa kutoa michango na hamasa zaidi 
– Kunahitajika vifaa zaidi vya kufundishia na kujifunzia ikiwa ni pamoja na vitabu, vifaa vya maabara n.k.
– Mabweni ya wavulana ambayo hayana umeme, yawekewe umeme ili wakati wa baridi wanafunzi wasipate shida ya kwenda mbali madarasani 
– Kuimarisha nidhamu ya masomo na mienendo miongoni mwa wanafunzi – Kuongeza ubora wa maslahi wanayopata walimu (kumbuka Mwese ni kiasi cha kilometa 1,500 kutoka Dar es Salaam!)
Lakini kwa ujumla shule inapendeza na kutia moyo. Mtu aliyeishi Mwese miaka ya 20 kurudi nyuma, akifika hapo leo hii atapigwa na bumbuwazi. Kuna maendeleo makubwa.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

July 31, 2012 at 11:09 pm

Posted in Siasa na jamii

5 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. yes you have done. Hatutaiacha mwese bila kuibadilisha iwe na fikra pevu tunaomba uzifanyie kazi changamoto zetu. Tafuta wana mwese mje tena mlete changamoto tena na vijana wanawahitaji sana we
    shuleyetumwese@hotmail.co.uk
    pamoja sana kaka simba

    Like

    reuben

    August 1, 2012 at 5:11 pm

    • Ndugu Reuben

      Pamoja sana. Hamasa, nia ya dhati, kutoruhusu maendeleo yaliyokwishapatikana kutodidimia na mshikamano ndiyo vitakavyoisukuma mbele Mwese pamoja na Taifa letu hili. Asante sana. Ingawa hukuwepo, lakini nilijisikia nyumbani. Ninawashukuru members of the staff waliokuwepo. Salamu kwa wote.

      Like

      simbadeo

      August 2, 2012 at 1:24 am

  2. Taasisi ya shule ya Sekondari, hususan kwa sehemu kama Mwese ni bahati iliyoje? manufaa yake kwa jamii hayahesabiki, ni mengi tu manufaa.

    Nawahamasisha wana-Mwese kuipenda Mwese, kwa kutoa michango kwa namna au njia yoyote, mchango wa hali na mali.Mchango wa Mawazo kwa kuitumia miundombinu yoyote ukiwemo na utandawazi, ukiweza kuchangia mali n.k. kwa ufupi kadiri ya uwezo wako, na ni vema zaidi hii iwe tena na tena, mpaka iwe desturi yetu.

    Pamoja na kwamba wana-Mwese sasa hivi wametapakaa dunia yote, hususan Nchini Rwanda, ambako hata mimi ndiko niliko sasa hivi, Kila mwenye asili, aliyezaliwa au kuishi Mwese kwa kipindi cha kutosha hususan udogoni, naamini hataisahau, ashakum si matusi, labda kama ana walakini. Kwa sababu,kuisahau
    asili yako, eneo ambalo ni msingi wa maisha yako ni sawa na kuinyea kambi.

    Bwana Deo, Kama mwanataaluma, mwandishi wa habari na mwenye kipaji, ninakuomba tena, uifanye kazi hii ya kuijumuisha jamii ya Wana-Mwese hasawale wenye taaluma maridhawa, ili siku moja, PAMOJA SANA tuweze kuinufaisha Mwese kwa kupitia taasisi zake kama vile Sekondari hiyo.

    WASAALAM.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    December 2, 2015 at 5:26 pm

  3. NAFIKIRI BLOGU YAKO BWANA DEO, YAWEZA KUTUMIWA KAMA CHOMBO MUAFAKA KITAKACHOZAA MATUNDA BORA MBELENI.

    Like

    Rwaka rwa Kagarama.

    December 2, 2015 at 5:30 pm

    • Ndugu Rwaka Kagarama. Asante sana kwa maoni na changamoto. Kwa hakika ni wazo zuri na linalohitaji kufanyiwa kazi. Kwa kuanzia tunaweza kufikiri mambo ya wastani ambayo utekelezaji wake si mgumu sana. Mathalani, najua kwamba Shule ya Sekondari Mwese ina mahitaji makubwa ya vitabu. Pengine kupitia michango tunaweza kununua vitabu kiasi na kuvisafirisha kwenda kule. Vilevile, shule zetu zile za msingi bado zingalipo, nazo zina mahitaji kama hayo, na vilevile uchakavu wa majengo.

      Kwa hiyo, ni jambo linalowezekana kuanza kuleta tofauti — japo ndogo katika jamii ya Mwese. Mwalimu Reuben Swilla ni mtu mwenye ushirikiano mkubwa. Naamini yeye ni kiungo muhimu. Tukifanya kazi pamoja naye tutafanikiwa katika azma yetu. Pengine tuanze na kufanya sensa ya watu waliowahi kupita/kuishi Mwese na wenye nia ya kuchangia ili kwa pamoja tuweke utaratibu unaofaa, wa wazi lakini wenye kuleta tija.

      Asante tena kwa changamoto hiyo. Tushirikiane kadiri tunavyoweza.

      Pamoja sana.

      Deo Simba (Mjuu wa Mnyang’ombe)
      kakasimba@gmail.com

      Like

      simbadeo

      December 3, 2015 at 12:13 am


Leave a comment