simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwese … Shule za Msingi, unazikumbuka?

leave a comment »

Sehemu ya mandhari ya Shule ya Msingi Lugonesi

Mwalimu Mtilu wa Shule ya Msingi Lugonesi akiwa kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu.

Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Mwese ulio jirani kabisa na Shule ya Msingi Lugonesi

Baadhi ya miti iliyo katika eneo la Shule ya Msingi Mwese … Pengine ulishiriki kuipanda wakati ulipokuwa mwanafunzi hapa?

Baadhi ya madarasa katika Shule ya Msingi Mwese …

Majengo mengine ya madarasa ya Shule ya Msingi Mwese …

Unapoingia Shule ya Msingi Lwega …

Pengine ulisoma kwenye moja ya shule hizi. Hivi sasa wewe ni mtu mzito mahali fulani hapa duniani. Kwa ufupi, majengo ya shule hizi yamechakaa sana. Ni majengo ya miaka mingi. Yaelekea bajeti ya Wizara ya Elimu imekuwa finyu kwa miaka mingi na kwa hiyo hakuna fedha za majengo zilizopelekwa Mwese. Sina hakika kama Mbunge wa eneo hili anajua hali hii. Lakini ujumbe muhimu kwako uliyewahi kusoma katika moja ya shule hizi ni kwamba ukumbuke kuwa una wajibu. Rejesha japo sehemu ndogo sana na mapato yako ya sasa katika maendeleo ya shule hizi. Mathalani, unaweza kuchangia kununua vitabu, unaweza kuchangia ukarabati wa baadhi ya majengo. Unaweza kufanya chochote kadiri unavyoguswa. Sote tuna wajibu wa kukumbuka tulikotoka. Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

July 28, 2012 at 11:56 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: