simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Changamoto za maisha … vijijini

with 2 comments

Afya. Gari la wagonjwa likiwa limekata chuma kinachounganisha gurudumu la mbele. Safari ilikomea hapo. Kwa bahati umbali kufika mjini ulibaki kama km 25 hivi, kwa hiyo mgonjwa alimalizia safari yake kwa gari lingine lililokuwa likipita hapo.

Maji. Miundombinu bado ni hafifu. Hivi ni kipi kinachotuzuia kutumia miundombinu kama hii iliyowahi kujengwa tangu miaka ya nyuma? Kwa nini wananchi waachwe kuendelea kuteseka kwa kwenda kutafuta maji mbali wakati tenki kama hili lingewapunguzia adha hiyo?

Kipato. Ni vigumu kuendesha maisha ya maana pasipo kipato cha uhakika. Je, vipi kuhusu haki za mtoto aliye mgongoni hapo? Nchi ina wajibu wa kuleta mabadiliko ya maana kwa wananchi kama huyu.

Elimu. Katika maeneo mengi hakuna madarasa ya maana. Kwa hiyo, hata watoto wanapofika umri wa kwenda shule hakuna mahali wanapoweza kwenda. Katika kijiji kimojawapo kuna vijana walioamua kujitolea kufundisha watoto. Kila mzazi anapaswa kulipa walau Sh1,000 kwa mwezi. Hata hivyo, wengi huwakatisha watoto wao masomo kwa kushindwa kumudu kiwango hicho … au pengine kwa kutoipa elimu kipaumbele. Hamasa na elimu kwa watu wazima ni muhimu ili watoto wapate fursa nzuri zaidi za kusoma.

Vitabu. Uhaba mkubwa. Kwenye darasa hilo kulikuwepo vitabu viwili tu. Mahitaji ya elimu yatakidhiwa vipi kwa mwendo huu? Kiu cha elimu ni kikubwa. Ukame wa vitabu, madarasa, walimu, madawati na vifaa vingine ni mkubwa mno.

Advertisements

Written by simbadeo

July 26, 2012 at 10:31 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Natumaini wahusika wanasoma blog hii na kuyapa uzito unaostahili masuala haya ya huduma za msingi vijijini.

  Like

  Magoti

  July 27, 2012 at 12:58 pm

  • Pengine wanachoona ni namna gani watawachuna zaidi ili wao binafsi wazidi kuneemeka. Pengine wanaojali ni wachache … maana wao wakiugua mara moja safari ya India au Afrika ya Kusini. Elimu ya watoto wao ni huko ughaibuni. Huduma ya maji wengine wanafuata utaratibu wa Charles Njonjo … bottled mineral water from the UK. Kipato/Ajira ya watoto wao wanapeana katika maltinational companies wanazoingia nazo ubia kuipora nchi rasilimali zake. Ndugu Magoti. Tuna safari ndefu bado. Ukombozi bado. Uhuru bado. Mapambano yanaendelea.

   Like

   simbadeo

   July 27, 2012 at 10:58 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: