simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Sauti za wananchi … Nairobi Mitaani

leave a comment »

“MY VOTE, MY VOICE, MY RIGHT” … pengine si nukuu ya moja kwa moja kutoka kwenye ujumbe ulio hapa kwenye kazi hii ya sanaa (michoro), lakini ndivyo ninavyoweza kuhitimisha kile kilichoingia akilini mwangu. Wananchi wanazungumza, wananchi wanaeleza hisia na matarajio yao. Kama wasipoandamana barabarani basi watatafuta njia nyingine ya kufikisha ujumbe wao. Wanawalenga viongozi wao. Kama wewe ni kiongozi — katika ngazi yoyote ile — Je, unasikiliza sauti ya watu? Unajua wanataka nini? Je, unajua kwa nini walikuchagua wewe na si mwingine? Unadhani hawana nguvu juu yako? Unafikiri kwamba kwa kuwa kwako kiongozi basi ndiyo umefika?

Kama wewe ni kiongozi, jichunguze vema. Unatumia nafasi yako kugawanya au kukusanya? Je, unawaleta watu pamoja au unaishia kuwatawanya kwa kuwavuruga na kuwanyima haki zao (kwa kuzikalia au kuzipuuza)? Jitafakari. Jitambue. Je, unakwenda Bungeni ili kulialia tu au unawakilisha kile ambacho watu wengi wanataka? Je, unatetea uzembe … ufedhuli … uharamia … ubaguzi … unyanyasaji … upotoshaji wa ukweli au ukengeuke mwingine? Wananchi wanaona … hata ujifiche nyuma ya mali nyingi kiasi gani. Funguka watumikie watu nawe utaneemeka hata baada ya kwenda kaburini. Ndiyo ujumbe kutoka mitaa ya Nairobi.

Advertisements

Written by simbadeo

July 10, 2012 at 11:36 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: