simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ulaya inafufuka upya katika kuinjilisha? … Hapa ni Dar!

leave a comment »

Mfasiri akiwaunganisha wainjilishaji waliotumia lugha ya Kiingereza na wazungumzaji wa Kiswahili.

Nikiwa kwenye mbio, nimewakuta maeneo ya Tazara karibu na kiwanda cha Bakhressa. Kwa mujibu wa kipeperushi chao, wao ni Bendi ya Sherehe za Huduma ya SOS kutoka Sweden. Tangu tarehe 13 Juni wapo viwanja vya Jangwani wakiendesha Mkutano Mkubwa wa Sherehe za Ishara na Miujiza. Kesho Jumapili ndiyo wanahitimisha.

Hapa walikuwa wakitoa burudani kwa kuimba na kuigiza ili kuwahamasisha watu washiriki kwenye mkutano huo wa kesho pale Jangwani.

Mhubiri kiongozi ni Johannes Amritzer wa Kanisa la SOS la Stockholm, Sweden.

Kwa taarifa zaidi qasiliana nao kupitia: signsandwondersfestival_dar@vcc.or.tz au wasiliana nao kwa simu No. 0714 503 638 au 0762 441 719.

Nilijiuliza: Siku hizi Ulaya inaamka tena kwa Injili? Maana wote hawa ni vijana, na tunasikia jinsi vijana Ulaya walivyomweka Mungu kapuni. Katika maigizo yao, kuna mmoja aliigiza kama mtesaji, na alivalia mavazi meusi, je, shetani (watu wabaya) ni mweusi?

Swali la uchokonozi wa kidini:
Kama kila Mtanzania atakuwa Mkristo, au kama kila Mtanzania atakuwa Mwislamu, au kama kila Mtanzania atageukia dini za kimila … Je, matatizo tuliyo nayo … wizi, ujambazi, ufisadi, umalaya, matusi, ugomvi, kutukanana, usaliti, kutowajibika, kukosa uaminifu n.k. yataisha mara moja? Wewe msomaji una maoni gani? Hebu tuitazame Somalia (99.9 asilimia ni Waislamu), Northern Ireland (Asilimia 99.9 ni Wakristo), Mexico (asilimia 95 ni Wakristo) … lakini wamegubikwa na matatizo kibao ya vita, dawa za kulevya n.k.

Kwa kifupi, je, dini hizi ndiyo jibu kwa matatizo yanayomkabili binadamu wa zama zote? Nina mashaka. Binafsi hufikiri kwamba kuna nyakati ambapo dini zimekuwa ndiyo vyanzo vya matatizo na migogoro. Nafikiri kuwa binadamu unayefikiri nje ya boksi ndiyo inaweza kuwa suluhu ya changamoto zetu. Karibu. Kama una maoni ya kutoa, tafadhali tumia lugha yenye staha kwako binafsi na kwa wengine.

Advertisements

Written by simbadeo

June 16, 2012 at 1:48 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: