simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Zilizosisimua … Habari

leave a comment »

Ushindi wa Mh John Mnyika, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, katika kesi iliyofunguliwa dhidi ya ushindi wake alioupata mwezi Oktoba 2010. Kwa mujibu wa maoni na mijadala katika vyombo vya habari vya kiraia, uamuzi wa mahakama umepokewa kwa mikono miwili. Pengine kulikuwa na swala la saikolojia pia nyuma yake. Ushindi huo umesaidia kupunguza fedheha. Kama angalishindwa … basi bila shaka jiji la Dar es Salaam lingekuwa kwenye fadhaa kubwa. Wengi waliamini kwamba matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2010 yalikuwa sahihi. Kwa Taifa … pengine matokeo hayo ni ushindi, ushindi mkubwa. Hebu fikiria kama ingekuwa lazima kurudia uchaguzi … fedha kiasi gani kingetumika, je, kwa gharama ya nani? Mungu ibariki Tanzania yetu tupate HEKIMA zaidi.

Kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Young Africans (Yanga) Bw Llyod Nchunga. Mara nyingine yatupasa kuchukua uamuzi mgumu wa kutuumiza wenyewe kwa maslahi ya walio wengi. Pongezi nyingi kwa Nchunga. Bila shaka halikuwa jambo rahidi kufikia ulipofikia. Lakini kwa maslahi ya Klabu ya Yanga, wanachama wake, ulimwengu wa soka la Tanzania na Watanzania … umeamua kuachia ngazi. Naamini umeonyesha mfano si katika ulimwengu wa soka tu bali hata katika maeneo mengine. Huwa tunasikia/tunaona mara nyingi tu jinsi watu wanaotuhumiwa kwa hili ama lile wanavyochelewa kuchukua uamuzi wa kukaa kando. Bw Nchunga, niseme tu kwamba umetupa somo kubwa. Pamoja na hilo, blogu hii inawatakia Yanga kila la kheri katika kujijenga upya ili kuleta ushindani utakaosaidia kukuza soka la Tanzania kwa ujumla.

Picha zote kutoka Mjengwablog.

Advertisements

Written by simbadeo

May 24, 2012 at 11:31 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: