simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Central Railway Line … Mwakyembe una kazi

with 2 comments

Hali halisi ya njia ya reli pale Gerezani … mita chache kutoka Makao Makuu ya Shirika la Reli Tanzania.

Reli imetitia kwenye udongo …

Kweli? Namna hii?

Hivi karibuni Shirika la Reli Tanzania (TRL) limetangaza kurejesha huduma ya usafiri wa reli kwa abiria — Reli ya Kati. Hata hivyo, kamera yetu ilikuta hali kama inavyoonekana hapo juu siku chake tu baada ya tangazo hilo kutoka. Tunauliza … endapo kipande hicho cha reli ambacho kipo yapata mita 800 tu kutoka yalipo Makao Makuu ya Shirika hilo kina hali hiyo … vipi hali ya njia ya reli huko mbele ya safari? Je, kwa uzito wa treni … inaweza kweli kupita maeneo kama haya kwa usalama? Labda inaweza kupita mara ya kwanza … na ya pili … na ya tatu … na ya kumi … lakini je mara ya hamsini? Ikitokea ajali … ni yaleyale KAZI ya MUNGU?

Ujumbe kwa Mh. Harrison Mwakyembe, waziri mpya mwenye dhamana ya usafirishaji ikiwamo ule wa reli … chonde chonde … ufufuaji miundombinu ya reli iendane sambamba na kuzifanya njia hizo zipitike kwa usalama unaoaminika … siyo ule wa kudra ya Mwenyezi Mungu. Ikitokea ajali katika hali ya namna hii … tumejihujumu wenyewe na wala si mtu mwingine. Reli ni njia kuu muhimu ya kufufua uchumi wa taifa hili. Kupitia reli … gharama za maisha mikoani zitakuwa na nafuu … maana gharama za usafirishaji zitakuwa chini. Maisha bora kwa Watanzania walio wengi yatawezekana kwa kufufua na kuimarisha usafirishaji wa reli.

Barabara, sawa tunazihitaji na tuendelee kuzijenga … Lakini reli ni ROHO … Ndiyo mkombozi wa mtu wa kawaida wa mikoani na hata yule wa mjini … Kupitia reli nchi inaweza kupunguza kasi ya ongezeko la bei za bidhaa mbalimbali, hususani zile za vyakula na nyinginezo.

Reli kwa maendeleo ya Taifa!!!

Advertisements

Written by simbadeo

May 20, 2012 at 10:31 am

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. ha ha haaaa, umenikumbusha , juzi niliona watu hapo katikati ya reli sijui ni maeneo gani wanatia mchange kwenye njia ya reli ili treni iweze kupita imaginge! kama wakati ule wa kukimbizana na magogo ya kuni kuchochea ili gari moshi liongeze kasi.
  ni kweli kabisa miundo mbinu na utengenezaji wa gari moshi lenyewe, vinginevyo hatutaziba ufa wala kujenga ukuta wa usafiri..

  Like

  jennifer

  May 21, 2012 at 1:19 pm

  • Jennifer, umenena. Bato tuna safari ndefu kama ya kutoka Pwani hadi Kigoma … mwisho wa reli.

   Like

   simbadeo

   May 23, 2012 at 10:11 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: