simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ujasiriamali … Mabibo Hosteli

with one comment

Jumatano tarehe 9 Mei hadi Alhamisi 10 Mei, kulikuwa na mafunzo kwa wajasiriamali yaliyoendeshwa na kitengo kinachohusika kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliendeshwa katika jengo la biashara lililo katika Hosteli za Mabibo, jijini Dar es Salaam. Sanjari na mafunzo wajasiriamali walitumia fursa hiyo kuonyesha bidhaa zao.

Vitabu ni baadhi ya bidhaa zilizokuwepo. Vilivyo vingi ni vile vilivyohusu ujasiriamali na namna ya kujitengenezea fedha zaidi.

<

Naam, akionyesha bidhaa za vitabu na machapisho mbalimbali.

Bwana Tito Oswady Nyaluke kutoka Soko Matola Mbeya alikuwepo kuonyesha bidhaa mbalimbali zinazotokana na mimea.

Wajasiriamali wanazidi kuleta mbinu bora zaidi. Hivi sasa unaweza kupata kisamvu kilicho kwenye vifungashio maridadi kabisa … Si kisamvu tu bali hata bidhaa nyingine za mimea vikiwamo vyakula. Big up sana.

Bibi Harriet Chamvanga naye alikuwepo ili kuonyesha bidhaa za sabuni za maji zinazotokana na mimea na maua mbalimbali. Umri si kikwazo cha kuendelea kujipatia kipato — na kuongeza mapato.

Akina dada wakitazama bidhaa zilizotengenezwa na wajasiriamali … kuna dawa zinazotokana na mimea ya asili pamoja na sabuni za kuogea na kufulia.

Mbegu zinazotoka kwenye mti wa mlonge. Kwa maelezo ya mwuzaji, hizo husaidia sana kutibu tatizo la figo kiasi cha kumaliza tatizo la kwenda haja ndogo karibu karibu.

Ujasiriamali unatuonyesha kwamba Watanzania tunaweza kuendelea. Kila mmoja anacho cha kumwuzia mwingine. Pengine kwa kutumia utaratibu huu wa uzalishaji na ubadilishanaji mali, tunaweza kuondokana na utegemezi kwa mataifa ya nje. Ni muhimu tukubali katika nafsi zetu kwamba TUNAWEZA.

Advertisements

Written by simbadeo

May 12, 2012 at 11:57 pm

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Halo KakaSimba. Mwenziyo natafuta mbegu hizi za Mlonge kuotesha. Naomba msaada. Kunayo njia waeza niunganisha na hao wakuzaji wa mti huu? Nitashkuru mpaka mwisho 🙂

    Like

    Lily Asili

    March 31, 2013 at 11:55 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: