simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Airtel … mng’aro

leave a comment »

Ni katika makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Kawawa, eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam. Ni uwekezaji wa maana. Uwekezaji unaotoa ajira kwa maelfu ya watu … moja kwa moja na kwa njia zisizo za moja kwa moja.

Hakuna ubishi kwamba huduma ya mawasiliano imepiga hatua kubwa sana. Moja ya hatua zilizopigwa ni pamoja na kupunguza gharama za kupata habari. Wale wa kizazi changu watakumbuka kwamba zamani zile kama unataka kuwasiliana na mtu, say, yeye anaishi Ubungo, na wewe unaishi Ilala, basi ilikulazimu kusafiri hadi Ubungo. Hapo, fikiria: unatumia nauli (kwa gharamza za sasa hivi mathalani si chini ya mia 600 ili ufike Ubungo kutoka Ilala), na zaidi sana unatumia sio chini ya saa 4 ili kutimiza azma yako hiyo. Siku hizi, mawasiliano yapo kwenye ncha za vidole. Papo hapo unampigia, unazungumza naye ulichotaka kuzungumza na mambo yanakwisha. Unaokoa gharama. Unaokoa muda.

Lakini, mabadiliko haya pia yanatugharimu kijamii. Mawasiliano ya kwenye simu na yale ya kuonana ana kwa ana ni tofauti. Ana kwa ana mnazungumza mengi zaidi. Kuna hata yale mawasiliano yasiyotumia maneno lakini yanayoeleza na kufafanua kile mwingine anachokizungumza — hayo huwezi kuyapata kupitia simu.

Kwa hiyo, hata sasa tunahitaji ‘balancing’ ili kwamba tusipoteze kabisa physical contacts kwa sababu kuna simu.

Tafakari ya leo. Pengine wewe pia una maoni kuhusu mawasiliano ya siku hizi kwa kulinganisha na mawasiliano ya kizamani. Yamimine hapa maoni hayo.

Advertisements

Written by simbadeo

May 6, 2012 at 9:54 am

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: