simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dala dala … Unatumiaje muda?

leave a comment »

Ndiyo. Ninauliza, unapotumia usafiri wa umma (dala dala) unatumiaje muda wako? Mathalani, umepata kiti, safari yako itakuchukua muda wa dakika 30 au 45, na kwa sababu ya foleni za Dar, basi pengine itakuchukua saa nzima. Je, muda huo wote huwa unafanya nini? Unasinzia? Unashangaa abiria wenzako – wakiwa katika maumbo tofautitofauti, mitindo ya nywele ya akina mama, mitindo ya mavazi? Unashangaa mazingira dala dala linamopita – mitaa, majengo, watu, masoko, maduka n.k.?

Pichani hapo juu kuja moja ya njia za kutumia muda wako VIZURI unapokuwa kwenye dala dala na umepata siti. SOMA. Soma kitabu. Soma gazeti – liwe pendwa au lile siriasi – SOMA. Kwa uzoefu wangu, tunatumia muda mwingi sana barabarani. Fikiria, saa nzima kwenda kazini, saa nzima kurudi. Hiyo ni saa mbili. Kwa kiwango cha kawaida cha kusoma. Utakuwa umesoma kurasa walau ishirini katika saa mbili. Ina maana kwamba unahitaji wiki moja tu kumaliza kusoma hadithi ya kurasa 120. Kumbe kila wiki ukijiwekea kusoma kitabu kimoja – au basi walau kila mwezi, ina maana kwamba katika mwaka mzima utakuwa umesoma vitabu visivyopungua kumi vya ukubwa wa wastani.

Jamani, tusome. Tusisingizie kwamba hatuna muda wa kusoma. Muda upo, muda tunao. Tunachohitaji ni kuondokana na uvivu na kujihurumia. SOMA. SOMA. SOMA.

Advertisements

Written by simbadeo

May 1, 2012 at 12:17 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , , , , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: